Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kijana kutoka Tanzania atumia stadi alizozipata kuwezesha vijana wenzake

Kijana kutoka Tanzania atumia stadi alizozipata kuwezesha vijana wenzake

Pakua

Lengo namba nane la malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya Umoja wa Mataifa linaangazia uchagizaji wa ukuaji uchumi endelevu na jumuishi na ajira yenye matokeo na kazi inayozingatia utu kwa wote.Katika kuangalia hatua zilizopigwa kufikia lengo hilo, takwimu zinaonyesha kuwa ukosefu wa ajira ulikuwa ni asilimia 5.7 mwaka 2016 huku idadi ya wanawake wasio na ajira ikiwa ni zaidi ya wanaume katika umri mbali mbali. Kuna uwezekano mara tatu zaidi ya vijana kutokuwa na ajira ikilinganishwa na watu waliokomaa, isitoshe nchi zaidi ya asilimia 76 zilizo na takwimu, kijana mmoja ndani ya kumi hawako katika sekta ya elimu na hawafanyi kazi. Lakini kwa upande mwingie vijana wamechukua mwamko kuwa sio lazima kusubiri mtu kuajiriwa. Ni kwa muktadha huo ambapo Tumaini Anathory wa radio washirika Karagwe FM wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera amezungumza na kijana mjasiriamali ambapo kwanza anaanza kwa kujitambulisha.

 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/Anathory Tumaini
Audio Duration
4'47"
Photo Credit
UNIDO