Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi ya PGWOCADE na harakati za kumkomboa msichana mkoani Rukwa Tanzania.

Taasisi ya PGWOCADE na harakati za kumkomboa msichana mkoani Rukwa Tanzania.

Pakua

Mojawapo ya vikwazo vya harakati za kumwinua mwanamke kutoka katika hali duni iliyodumu tangu enzi na enzi mila na desturi za baadhi ya maeneo duniani ambayo wanajamii wamekwenda kwa kasi ndogo katika kuziacha mila hizo kandamizi na potofu. Licha ya ugumu huo, bado mazingira hayo hayapaswi kuwa kikwazo kwa wanarahakati ambao wanahaha kufikia  usawa wa kijinsia kwani mabadiliko ya mila na desturi hayawezi kuwa ya siku moja.

Mkoani Rukwa nchini Tanzania taasisi ya Practice for Girls and Women Career Development (PGWOCADE) inafanya harakati za kupambana na mila zinazokwamisha mstakabali wa wanawake na tayari imeweza kuwafikia zaidi ya wasichana 3000 katika shule 34 mkoani humo. Katika mahojiano na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa taasisi hiyo Bi Jackline Tung’ombe anaeleza hali ilivyo mkoani Rukwa na namna wanavyoishughulikia.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Stella Vuzo/Jackiline Tung'ombe
Audio Duration
4'27"
Photo Credit
Photo: IRIN/Mujahid Safodien