Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazina mipaka- mkaazi Bunyoro-Uganda

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazina mipaka- mkaazi Bunyoro-Uganda

Pakua

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linachagiza mataifa kuchukua hatua za haraka ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Lengo hilo limeorodhesha malengo madogo ambayo yatasaidia katika kufanikisha SDG 13 ifikapo mwaka 2030. Katika kupima utekelezaji wa lengo hilo, moja ya hatua ni kuimarisha uwezo wa kupanga na kusimamia mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika nchi maskini, visiwa vidogo na zile zinazoendelea, ikiwemo kwa kulenga wanawake,vijana na jamii mashinani na zilizotengwa. Mfano wa jamii mashinani ambazo zinashuhudia mabadiliko ya tabianchi ni katika eneo la Bunyoro nchini Uganda kama anavyosimulia John Kibego katika makala ifuatayo.

 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'41"
Photo Credit
UN News/ Anton Uspensky