Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakazi wachukua hatua kulinda mto Nkumara Uganda

Wakazi wachukua hatua kulinda mto Nkumara Uganda

Pakua

Maziwa, hifadhi za maji na mito vyote vina umuhimu mkubwa si tu kwa mazingira bali pia binadamu wanaozingira vyanzo hivyo vya maji. hata hivyo licha ya vyanzo hivi kuwa na umuhimu mkubwa kiuchumi, kimazingira na kiutamaduni bado vinakabiliwa na athari kutokana na shughuli za binadamu ambazo zinaweza kusababisha uharibifu wa vyanzo hivyo. Ulinzi kutokana na shuhguli hizo ni muhimu na ni kwa mantiki hiyo ambapo wakazi wa mto Nkumara nchini Uganda ambao wamechukua hatua kuandika katiba katika kuhakikisha ulinzi wa mto huo. Je kulikoni? Ungana na John Kibego katika Makala ifautayo.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/John Kibego
Audio Duration
3'57"
Photo Credit
IOM/Amanda Nero