Skip to main content

Dau la plastiki kusafiri kutoka mji mkongwe wa Lamu hadi mji mkongwe Zanzibar kuchagiza kuhusu madhara ya taka za plastiki

Dau la plastiki kusafiri kutoka mji mkongwe wa Lamu hadi mji mkongwe Zanzibar kuchagiza kuhusu madhara ya taka za plastiki

Pakua

Dau la kijadi lililotengenezwa na taka za plastiki zilizookotwa pwani ya Kenya na miji mbalimbali litaanza safari yake ya kwanza tarehe 24 mwezi huu kutoka mji mkongwe wa Lamu nchini Kenya hadi mji mkongwe huko Zanzibar nchini Tanzania tarehe 7 mwezi ujao, ikiwa ni safari ya umbali wa kilometa 500.

Katika safari hiyo dau hilo litapita na kusimama maeneo mbalimbali ili kuelimisha jamii kuhusu madhara ya taka za plastiki. Na Je nini lengo la dau hili? Kwa nina basi Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili amezungumza na Clara Makenya, mwakilishi wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha/Clara Makenya
Audio Duration
5'53"
Photo Credit
UN Environment