Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/Tanya Bindra

Mwanamke ajikwamua kwa juhudi zinazojali mazingira, Uganda

Wakati ulimwenguni kukishuhudiwa mabadiliko ya tabianchi na athari zake Umoja wa Mataifa unahimiza nchi na watu binafsi kushiriki katika kuyalinda mazingira kwa njia mbali mbali ikiwemo kugeuza athari kuwa faida. Uchafuzi wa hewa na ukataji miti ni miongoni mwa changamoto ambazo zinajitokeza katika utunzaji wa mazingira. Lakini nchini Uganda baadhi ya watu wameanza kupata mwamko na kutambua kuwa wasipohifadhi mazingira leo basi vizazi vya kesho viko mashakani. Miongoni mwao ni mwanamke mmoja aliyeamua kutumia nishati mbadal ambayo inajali mazingira, kulikoni?

Sauti
3'48"
World Bank/Simone D. McCourtie

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kujiendeleza

Mchango wa vijana katika kusongesha ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ni dhahiri. Ni kwa kutambua hilo ndio maana Umoja wa Mataifa  kupitia mashirika yake mbalimbali na wadau unaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika maenedeleo ya kijamii.  Nchini Tanzania vijana wameitikia wito huo  na kuchukua hatua na miongoni mwao ni Paschal Masalu  ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa liitwalo ElimikaWikiendi ambalo linawahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kujiendeleza. B

Sauti
4'18"
FIB/MONUSCO

Ninapoona wanawake wana amani hiyo inanipa hamasa kuendelea kuwasaidia- Private Deborah

Umoja wa Mataifa  umekuwa kila uchao  ukipaza sauti kuhusu umuhimu wa uwepo wa walinda amani wanawake kwenye vikosi vya ulinzi wa amani vya chombo hicho. Tangu mwaka jana Umoja wa Mataifa uliweka bayana kuwa uwepo wa wanawake kwenye vikosi hivyo una mchango mkubwa katika siyo tu kufanikisha majukumu ya ulinzi wa amani bali pia kuwezesha wanawake walio kwenye mizozo kuwa wazi na wanawake wenzao katika kuwaeleza changamoto wanazokabiliana nazo na pia kufundishwa stadi za kujikwamua kimaisha.

Sauti
4'
© UNHCR/Diana Diaz

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa vitendo.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje. Nchini Tanzania, moja ya mataifa yaliyoridhia malengo hayo, jeshi la wananchi, JWTZ limeitikia wito huo kupitia shule ambazo inazimiliki. Luteni Kanali Semunyu wa JWTZ alishiriki kikao kilichosheheni maofisa wa ngazi mbalimbali za kijeshi pamoja na wale wanaoongoza taasisi za elimu zilizoko chini ya JWTZ.

Sauti
4'53"
©FAO/Laure-Sophie Schiettecatte

Uendelevu wa uhakika wa chakula wamulikwa, Uganda

Ukosefu wa uhakika wa chakula na lishe hutokea wakati watu wanakosa fursa ya kuchagua, wanakuwa na wasiwasi kuhusu kuishiwa na chakula na wanalazimika kubadilisha ratiba ya kupata mlo kwa sababu za kiuchumi.

Kwa mujibu wa shirika la chakula Na kilimo duniani, FAO, hili linaweza kutokana na umaskini, mazao duni au mabadiliko ya tabianchi. FAO inasema ili kufikia uhakika wa chakula inamaanisha kupata chakula bora na endelevu na kwa viwango sahihi kwa ajili ya watu katika kaya.

Sauti
3'47"
UNIC/Stella Vuzo

Mahojiano yangu na Idhaa ya Kiswahili ya UN yamenifungulia njia: Kijana Idd

Dunia imeendelea kukumbwa na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira kama ukataji miti hovyo.

Ni katika kipindi hiki ambapo kote duniani kila mtu anahamasishwa popote pale alipo afanye lolote awezalo ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi kama vile ongezeko la joto duniani au baridi kali   vitokanavyo na uharibifu wa mazingira.

Sauti
3'59"
UNICEF/Prashanth Vishwanathan

Likizo ya uzazi ni haki ya mama na mtoto: Doris Mollel

Likizo ya uzazi ni haki kwa kila mama anayefanyakazi kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na ni muhimu katika afya ya mama na mtoto lakini zaidi ukuaji wa mtoto. Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la kazi duniani , ILO lililopisha mkataba wa likizo ya uzazi mwaka 1919, suala hili limekuwa changamoto kwa mamilioni ya wazazi katika nchi nyingi duniani kutokana na sheria za kazi zilizowekwa na waajiri wao.

Sauti
5'36"
UNDP Tuvalu/Aurélia Rusek

Wanajamii wana majibu sahihi kuhusu changamoto za uharibifu wa mazingira- Dkt Elifuraha Lalitaika.

Kila uchao ripoti za watu wa asili kufurushwa kwenye maeneo yao ya asili kwa sababu ya kuimarisha uhifadhi wa mazingira au kuepusha watu wa jamii hizo kuharibu maeneo hayo, zimekuwa zikisika. Matukio haya ni kuanzia Afrika hadi Ulaya, Amerika hadi Asia bila kusahau Amerika ya Kusini. Katika maeneo mengine, watu hao hufurushwa kwa ajili ya kufanikisha miradi inayodaiwa kuwa ni ya maendeleo huku watu wa jamii ya asili wakisalia bila mazingira ambayo wamezoea.

Sauti
3'42"
UNICEF/Frank Dejongh

Wadau mkoani Ruvuma nchini Tanzania na harakati za kusongesha afya ya mtoto

Shirika la afya duniani, WHO, linasema upatikanaji wa huduma ya afya ni changamoto katika mataifa mengi hususan yanayoendelea na hivyo ni muhimu kwa serikali na wadau kushirikiana katika kuhakikisha huduma hiyo inapatokana hasa kwa watoto. Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo zinazoendelea zinazojaribu kutumia mbinu mbalimbali kukabiliana na changamoto hizo za afya hususan kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu je nini kinafanyika?

Sauti
5'18"