Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano yangu na Idhaa ya Kiswahili ya UN yamenifungulia njia: Kijana Idd

Mahojiano yangu na Idhaa ya Kiswahili ya UN yamenifungulia njia: Kijana Idd

Pakua

Dunia imeendelea kukumbwa na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira kama ukataji miti hovyo.

Ni katika kipindi hiki ambapo kote duniani kila mtu anahamasishwa popote pale alipo afanye lolote awezalo ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi kama vile ongezeko la joto duniani au baridi kali   vitokanavyo na uharibifu wa mazingira.

Kwa kuzingatia hilo katika nchi mbalimbali watu wanachagizwa kuwa wabunifu na kugeuza athari kuwa manufaa. Nchini Tanzania kijana Idd Hamis aliitikia wito pale alipobuni wazo la kutengeneza mashine inayotumika kutengeneza mkaa utokanao na taka ngumu, mkaa ambao ni rafiki kwa afya ya binadamu na pia mazingira. Baada ya kuhojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kijana huyo anasema mradi wake umefanikiwa zaidi na kuweza kuwafikia vijana na wanawake wengi ambao nao sasa wamehamasika kutaka kujiunga na harakatai zake za kuyalinda mazingira.Akizungumza na Arnold Kayanda wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Idd anafafanua muendelezo wa jitihada zake na manufaa aliyopata.

Soundcloud

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Idd Hamisi
Sauti
3'59"
Photo Credit
UNIC/Stella Vuzo