Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uendelevu wa uhakika wa chakula wamulikwa, Uganda

Uendelevu wa uhakika wa chakula wamulikwa, Uganda

Pakua

Ukosefu wa uhakika wa chakula na lishe hutokea wakati watu wanakosa fursa ya kuchagua, wanakuwa na wasiwasi kuhusu kuishiwa na chakula na wanalazimika kubadilisha ratiba ya kupata mlo kwa sababu za kiuchumi.

Kwa mujibu wa shirika la chakula Na kilimo duniani, FAO, hili linaweza kutokana na umaskini, mazao duni au mabadiliko ya tabianchi. FAO inasema ili kufikia uhakika wa chakula inamaanisha kupata chakula bora na endelevu na kwa viwango sahihi kwa ajili ya watu katika kaya.

Kwa mujibu wa ripoti ya FAO kwa Uganda msimu mirefu ya ukame kumekuwa na athari katika uzalishaji katika miaka ya hivi karibuni. Mabadiliko hayo yamethibitishwa na wakazi wa Hoima nchini humo katika makala  ifuatayo ya John Kibego

Audio Credit
Patrick Newman/ John Kibego
Sauti
3'47"
Photo Credit
©FAO/Laure-Sophie Schiettecatte