Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ninapoona wanawake wana amani hiyo inanipa hamasa kuendelea kuwasaidia- Private Deborah

Ninapoona wanawake wana amani hiyo inanipa hamasa kuendelea kuwasaidia- Private Deborah

Pakua

Umoja wa Mataifa  umekuwa kila uchao  ukipaza sauti kuhusu umuhimu wa uwepo wa walinda amani wanawake kwenye vikosi vya ulinzi wa amani vya chombo hicho. Tangu mwaka jana Umoja wa Mataifa uliweka bayana kuwa uwepo wa wanawake kwenye vikosi hivyo una mchango mkubwa katika siyo tu kufanikisha majukumu ya ulinzi wa amani bali pia kuwezesha wanawake walio kwenye mizozo kuwa wazi na wanawake wenzao katika kuwaeleza changamoto wanazokabiliana nazo na pia kufundishwa stadi za kujikwamua kimaisha. Miongoni mwa wanawake walinda amani ni Private Deborah Mabula ambaye anahudumu katika kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa  Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Katika mahojiano kwa njia ya simu na Assumpta Massoi kutoka Beni, DRC anaelezea mchango wao wanawake walinda amani katika kusaka amani ya kudumu na endelevu nchini DRC. 

Soundcloud

 

 

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'
Photo Credit
FIB/MONUSCO