Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira yaweza kuwakomboa wanawake -Grassroot Women Initiative Network

Mazingira yaweza kuwakomboa wanawake -Grassroot Women Initiative Network

Pakua

Wanawake katika sehemu mbali mbali duniani wanajikita katika mbinu tofauti kwa ajili ya kubadilisha maisha yao na ya jamii wanakoishi na kwingineko hususani mazingira yanayowazunguka. Mmoja wa wanawake walioamua kuchukua jukumu la kubadili hali ya wakazi wa mtaaanakokuita nyumbani ni Beatrice Wanjiru. Bi. Wanjiru kutoka taasisi ya Grassroot Women Initiative Network anafanya kazi mtaa wa Kayole jijini Nairobi nchini Kenya na kwingineko kwa ajili ya kuhakikisha jamii hususan wanawake na watoto wanapata haki za msingi ambazo ni kero kubwa ikiwemo haki ya maji safi. Bi Wanjiru akizungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii amemwelezea harakati zake za kupigania huduma ya msingi ya maji lakini anafafanua kwanza kazi ambazo wanajikita nazo kwa ujumla.

Soundcloud
Audio Credit
Flora Nducha/Beatrice Wanjiru
Audio Duration
3'55"
Photo Credit
Photo: IRIN/A. Morland