Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajamii wana majibu sahihi kuhusu changamoto za uharibifu wa mazingira- Dkt Elifuraha Lalitaika.

Wanajamii wana majibu sahihi kuhusu changamoto za uharibifu wa mazingira- Dkt Elifuraha Lalitaika.

Pakua

Kila uchao ripoti za watu wa asili kufurushwa kwenye maeneo yao ya asili kwa sababu ya kuimarisha uhifadhi wa mazingira au kuepusha watu wa jamii hizo kuharibu maeneo hayo, zimekuwa zikisika. Matukio haya ni kuanzia Afrika hadi Ulaya, Amerika hadi Asia bila kusahau Amerika ya Kusini. Katika maeneo mengine, watu hao hufurushwa kwa ajili ya kufanikisha miradi inayodaiwa kuwa ni ya maendeleo huku watu wa jamii ya asili wakisalia bila mazingira ambayo wamezoea. Ufurushaji wa watu wa jamii ya asili kwa njia moja au nyingine umesababisha kuharibika kwa bayonuai katika maeneo hayo ya asili ambapo Dkt Elifuraha Lalitaika  mhadhiri wa Chuo Kikuu nchini Tanzania na pia mtaalamu wa jukwaa la kudumu la watu wa asili la Umoja wa Mataifa anasema ni  jukumu la jamii za asili katika ulinzi huo. Hata hivyo anasema kunahitajika  mikakati ya kidunia na kwa hivyo ni muhimu kwamba changamoto zitokanazo na  athari za mabadiliko ya tabia nchi zichukuliwe kama   jukumu la kila mtu kwani hilo ni tatizo linaloshuhudiwa duniani kote. Je ni kwa vipi basi, Ungana basi na Grace Kaneiya katika makala hii ambayo mahojiano yake yamefanikishwa na kituo cha habari za Umoja wa Mataifa UNIC, jijini Nairobi, Kenya.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Grace Kaneiya/ Dkt Elifuraha Lalitaika
Sauti
3'42"
Photo Credit
UNDP Tuvalu/Aurélia Rusek