Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kujiendeleza

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kujiendeleza

Pakua

Mchango wa vijana katika kusongesha ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ni dhahiri. Ni kwa kutambua hilo ndio maana Umoja wa Mataifa  kupitia mashirika yake mbalimbali na wadau unaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwahimiza vijana kushiriki kikamilifu katika maenedeleo ya kijamii.  Nchini Tanzania vijana wameitikia wito huo  na kuchukua hatua na miongoni mwao ni Paschal Masalu  ambaye ni afisa mtendaji wa jukwaa liitwalo ElimikaWikiendi ambalo linawahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kujiendeleza. Baada ya kushiriki katika jukwaa la vijana  kwenye makao makuu ya Umoja huo New York Marekani mwaka jana , alirudi nyumbani Tanzania kushiriki kwa vitendo mafunzo waliyoyapta. Leo katika mahojianio na Patrick Newman wa Idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaanza  kuelezea hatua waliyopiga mwaka mmoja baada ya mafunzo kuhusu maendeleo ya vijana na mitandao ya kijamii.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Patrick Newman
Audio Duration
4'18"
Photo Credit
World Bank/Simone D. McCourtie