Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News

Afrika yapazia sauti mambo 6 COP25

Wakati mkutano huo wa COP25 ukiendelea mashirika ya asasi za kiraia kutoka barani Afrika yakiwakilisha nchi zaidi ya 40, chini ya mwamvuli wa Muungano wa Afrika wa haki na tabianchi (PACJA), yamedai jumuiya ya kimataifa kuchapuza mchakato na maamuzi yatakayozingatia mazingira na maslahi ya bara hilo .

Sauti
6'9"
UN News

Harakati za kupinga ukatili dhidi ya wanawake kwenye maeneo ya migodi Uganda zashika kasi

Siku 16 za kimataifa za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zikiendelea kuangaziwa duniani, ni wazi kuwa ukatili wa kijinsia ni changamoto ya ulimwenggu ukiwa na madhara makubwa kwa watoto wa kike na wanawake.  Nchini  Uganda uzinduzi wa filamu itwayo ‘Wanawake Hushikilia Anga’ ni miongoni mwa harakati za asasi za kiraia zilizofanyika nchini humo katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Je nini kimefanyika, ungana basi na John Kibego katika, ambaye amekuwa shuhuda wetu.

Sauti
3'32"
UNDP Bhutan/NPIF

IFAD yawezesha Bhutan kuendelea kupata mlo wao wa asili mezani

Mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 unaanza leo  huko Madrid, Hispania kuangazia hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa hatua sahihi za kulinda tabianchi zinatekelezwa, wakati huu ambapo ni miaka 4 sasa tangu kupitishwa kwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi. Hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na kupunguza hewa chafuzi na kuzingatia kilimo endelevu kisichoharibu mazingira sambamba na kilimo cha mazao ya asili.

Sauti
4'9"
UN News

Ni sisi wanawake tutakaoubadilisha msemo wa adui wa mwanamke ni mwanamke-Jonitha Nitoya Joram

Mabadiliko chanya katika jamii yanaweza kuanzishwa na mtu mmoja tu, hiyo ndiyo imani ya msichana Jonitha Nitoya Joram muhitimu wa Chuo Kikuu ambaye ameamua kuutumia muda wake wa ziada kuwaelimisha wasichana wenzake na wanawake wafanyabiashara nchini Tanzania ambao hawana elimu ya ujasiriamali. Joanitha anatoa wito kwa kila mtu katika jamii kusambaza kwa upendo maarifa aliyonayo ili kuweza kumkomboa kila mmoja katika jamii hususani wale ambao hawakujaliwa kuipata elimu. Arnold Kayanda wa UN News amefanya mahojiano na msichana huyu anayeanza kwa kueleza namna alivyoanza harakati hizo.

Sauti
3'33"
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya

Wanawake wa Zanzibar sasa wameamka katika ujasiriliamali: Barefoot

Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs inachagiza hatua zichukululiwe na kila mdau kuanzia serikali, makampuni binafsi asasi za kiraia na hata jamii kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma ifikapo 2030. Wito huo unaendelea kuitikiwa na kuleta manufaa katika jamii, mfano kisiwani Zanzibar nchini Tanzania chuo kisicho cha kiserikali cha miguu peku au Bare foot College ni moja ya wadau hao kikitoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yanayolenga  kumkomboa mwanamke. Miongoni mwa mafunzo hayo ni ya utengenezaji wa paneli za sola.

Sauti
4'11"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Mabadiliko ya mitaa yetu ya Mathare yataletwa na sisi wenyewe-Peter Otieno

Ikiwa imesalia miaka takribani kumi ili kufikia mwaka 2030 ambao ndio mwaka uliowekwa na ulimwengu kuwa malengo 17 ya maendeleo endelevu yawe yametekelezwa kikamilifu, juhudi zinaendelea kila kona kuhakikisha lengo hilo kuu linatimia. Mathalani, Kijana mmoja mzaliwa wa Mtaa wa mabanda wa Mathare mjini Nairobi Kenya, Peter Otieno amefanya uamuzi wa kuwaleta pamoja vijana wenzake ili waanzishishe mradi wa kusafisha mazingira ya mtaa wao kutokana na kero za mirundikano ya taka katika kila kona.

Sauti
4'7"
© UNICEF/UN0346146/Diefaga

Jamii inasemaje kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto?

Makala ya leo imejikita na mkataba wa haki za mtoto duniani uliopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa miaka 30 iliyopita ukisimamia nguzo kuu nne ambazo ni haki ya kutobaguliwa, kuhakikisha mahitaji yake yanatimizwa, haki ya kuishi na kuendelezwa na haki ya kusikilizwa. Na je tangu kupitishwa kwa mkataba huo, jamii, wazazi na watoto wenyewe wanauelewaje mkataba huo? Na una maana gani kwao? Ungana na Flora Nducha

 

Sauti
5'53"
UN News/Grece Kaneiya

Dhana niliyokuwa nayo kuhusu China ni tofauti na hali halisi-Mwalimu Gichana

Kwa kawaida taarifa kuhusu eneo au nchi hususan kupitia vyombo vya habari vinatoa taswira moja kuhusu eneo au nchi na wakati mwingine pia kuhusu watu wanoishi sehemu tajwa. Lakini mara nyingi inakuwa hiyo sio hali halisi. Na kwa mgeni wetu kwa makala ya leo, mwalimu Joseph Gichana mzaliwa wa Kenya taswira aliyokuwa nayo kuhusu China ni tofauti na hali aliyoshuhudia nchini humo ambako anafanya kazi na kuishi na familia yake. Kulikoni? Ungana na Flora Nducha na mwalimu Gichana akizungumzia maisha ughaibuni.

Sauti
3'50"