Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD yawezesha Bhutan kuendelea kupata mlo wao wa asili mezani

IFAD yawezesha Bhutan kuendelea kupata mlo wao wa asili mezani

Pakua

Mkutano wa 25 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP25 unaanza leo  huko Madrid, Hispania kuangazia hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa hatua sahihi za kulinda tabianchi zinatekelezwa, wakati huu ambapo ni miaka 4 sasa tangu kupitishwa kwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi. Hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni pamoja na kupunguza hewa chafuzi na kuzingatia kilimo endelevu kisichoharibu mazingira sambamba na kilimo cha mazao ya asili. Ni kwa kutumbua hilo, mpishi mashuhuri duniani kutoka Italia, Carlo Cracco ametembelea Bhutan kuona ni kwa vipi mabadiliko ya tabianchi yamelazimisha wakulima kuendana na mazingira ili kuendelea kulima mazao muhimu ya vyakula vya asilia vya taifa hilo la bara la Asia, harakati ambazo zinapigiwa chepuo na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD. Je nini ameshuhudia? ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'9"
Photo Credit
UNDP Bhutan/NPIF