Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wa Zanzibar sasa wameamka katika ujasiriliamali: Barefoot

Wanawake wa Zanzibar sasa wameamka katika ujasiriliamali: Barefoot

Pakua

Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs inachagiza hatua zichukululiwe na kila mdau kuanzia serikali, makampuni binafsi asasi za kiraia na hata jamii kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma ifikapo 2030. Wito huo unaendelea kuitikiwa na kuleta manufaa katika jamii, mfano kisiwani Zanzibar nchini Tanzania chuo kisicho cha kiserikali cha miguu peku au Bare foot College ni moja ya wadau hao kikitoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yanayolenga  kumkomboa mwanamke. Miongoni mwa mafunzo hayo ni ya utengenezaji wa paneli za sola. Kwa undani zaidi kuhusu mradi huo ungana na Flora Nducha na Pendo Yaredi Daudi mratibu wa chuo hicho anayeanza kueleza ni wanawake gani wanaowalenga

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Flora Nducha/Pendo Yaredi Daudi
Audio Duration
4'11"
Photo Credit
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya