Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya mitaa yetu ya Mathare yataletwa na sisi wenyewe-Peter Otieno

Mabadiliko ya mitaa yetu ya Mathare yataletwa na sisi wenyewe-Peter Otieno

Pakua

Ikiwa imesalia miaka takribani kumi ili kufikia mwaka 2030 ambao ndio mwaka uliowekwa na ulimwengu kuwa malengo 17 ya maendeleo endelevu yawe yametekelezwa kikamilifu, juhudi zinaendelea kila kona kuhakikisha lengo hilo kuu linatimia. Mathalani, Kijana mmoja mzaliwa wa Mtaa wa mabanda wa Mathare mjini Nairobi Kenya, Peter Otieno amefanya uamuzi wa kuwaleta pamoja vijana wenzake ili waanzishishe mradi wa kusafisha mazingira ya mtaa wao kutokana na kero za mirundikano ya taka katika kila kona. Mradi huo ambao sasa unafahamika kama Furaha Community Initiative umepanuka na kuwajumuisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na hivyo kuleta sura mpya ya mazingira katika sehemu za mtaa wao. Kufanikiwa kwa kijana Otieno si tu kunafanikisha lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa linaloangazia usafi wa mazingira, bali pia mafanikio hayo yatakuwa mtambuka na kugusa malengo mengine kama lile la 11 kuhusu miji na jamii endelevu.  Jason Nyakundi amekutana na Otieno ambaye anaaanza kwa kuelezea safari hiyo ya kuboresha mazingira.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Jason Nyakundi/ Peter Otieno
Audio Duration
4'7"
Photo Credit
UN-Habitat/Julius Mwelu