Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo cha kisasa na chenye tija miongoni mwa wakulima nchini Uganda

Kilimo cha kisasa na chenye tija miongoni mwa wakulima nchini Uganda

Pakua

Wakati mkutano wa 22 nchi  wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi ukiendelea mjini Marrakesh nchini Morocco, moja ya mada zinazojadiliwa ni kilimo endelevu , chenye tija na na ambacho kinahifadhi mazingira.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiongozwa na lile la chakula na kilimo FAO yameeleza umuhimu wa kilimo hai katika kupunguza uharibifu wa mazingira, ikielezwa kuwa shughuli za kilimo zinaathiri mazingira. Uharibifu huo ni kupitia matumzi holela ya ardhi, mbolea ya samadi n ahata za kawaida hutoa gesi chafuzi zinazokwangua ukanda wa ozone.

Rob Vos mkurugenzi wa maendeleo ya uchumi wa kilimo, FAO anasema ni kwa kuzingatia hilo ndio maana kwenye mkutano wa COP22 wanalenga nchi zifahamu..

( SAUTI YA VOS)

“Jinsi ya kuhakikisha sera zao za kilimo zinaendana na harakati za kulinda mazingira na jinsi ya kuanzisha mbinu bora na endelevu za kilimo.”

Nchini Uganda mwandishi wetu John Kibego amemtembela mkulima aliyefanikiwa kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo..

(PACKAGE KIBEGO)

Photo Credit
Fred Kwolekya akiwa nyumbani kwake.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Kibego)