Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wakimbizi wa ndani wafungasha virago mara ya pili Gaalkacyo:OCHA

Hebu fikiria baada ya kukimbia vita na kuwa mkimbizi wa ndani sasa walazimika kufungasha virago tena. Hali hiyo imewasibu aelfu ya wakimbizi wa ndani na wakazi wa mji wa Gaalikacyo katikati mwa Somalia wanaolazimika kunusuru maisha yao kufuatia machafuko yaliyozuka hivi karibuni.

Kwa mujibu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA watu kutoka jimbo la Galmadug na Puntland walizua tafrani mapema mwezi huu, hadi sasa watu takribani 20 wamepoteza maisha na maelfu kuzihama nyumba zao.

Wanunua mafuta ya elfu 50, washindwaje mtaji wa elfu 20? - TYIC

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo vijana kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Vijana walio katika ngazi mbalimbali za elimu wanachagizwa kutumia stadi walizo nazo ili kubadili maisha yao na kuondoa utegemezi wa kusubiri kuajiriwa. Miongoni mwao ni Jane Michael, mhitimu wa Chuo Kikuu nchini Tanzania ambaye sasa yuko kwenye kikundi cha vijana wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma, TYIC.

Mafunzo ya ngono kwa watoto Malawi sasa marufuku

Ndoa za utotoni, ni tatizo sugu katika maeneo mbali mbali duniani na huletwa na mila na desturi potofu. Ndoa hizi huwaathiri watoto kimwili, kisaikolojia na hata kimaendeleo, kwani wengi wao hushindwa kumaliza masomo na kuanza shughuli za kutunza familia. Nchini Malawi, harakati za kuharamisha ndoa hizo zinaendelea zikiambatana na kuwan'goa madarakani viongozi wa vijiji wasiozingatia amri. Je ni nani alie mstari wa mbele katika harakati hizi..basi ungana na Brian Lehander kufahamu zaidi katika makala hii

(MAKALA NA BRIAN LEHANDER)

Kuna nuru gizani, elimu kwa wakimbizi kutoka DRC

Kawaida maisha ya ukimbizini yanakuwa ni ya dhiki na taabu za kila aina. Lakini inaweza kutokea mkimbizi akafaidika kwenye maisha hayo ya kuomba hifadhi kwa njia moja ama nyingine. Hali ndivyo ilivyo kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walioko katika kambi ya Bwagiriza eneo la Ruyigi mashariki mwa Burundi. Licha ya masahibu ya maisha wanayokumbana nayo, baadhi ya wakimbizi watu wazima ambao awali hawakupata fursa ya

Umaskini ni zaidi ya kukosa pesa

Tarehe 17 Oktoba kila mwaka ni siku ya kuondoa umaskini duniani, moja ya malengo ya maendeleo endelevu. Umaskini unakwamisha kufanikishwa kwa malengo hayo na ndio maana Umoja wa Mataifa unataka hatua hizo zipatiwe kipaumbele. Nchini Tanzania harakati za kujikwamua kutoka lindi la umaskini nazo zinashika kasi kuanzia ngazi ya kaya hadi kitaifa, huku watu wakiwa na tafsiri tofauti ya neno umaskini.

Kauli ya msichana mwenye ndoto ni moto yathibitika UM

Mtoto wa kike! Ni lulu ambayo kila inapotaka kung’ara hukumbwa na utando wa kuikwamisha. Harakati za kuzuia kung’ara kwa kundi hilo kumesababisha watoto zaidi ya milioni 62 kote ulimwenguni kutokwenda shule. Sababu kama vile mila na desturi potofu, vita na hata ukata zinatajwa. Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia hilo, miaka mitano iliyopita ilitenga tarehe 11 mwezi Oktoba ya kila mwaka kuwa siku ya mtoto duniani. Katika maadhimisho ya mwaka huu, ngonjera zilishika kasi kuonyesha madhila na ndoto za mtoto wa kike, shuhuda wetu ni Brian Lehandar.

Kiwanda cha kuzalisha mende na funza kuokoa wafugaji Tanzania

Wiki ya vijana imefunga pazia huko nchini Tanzania, tukio ambalo liliandaliwa kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na serikali ya Taifa hilo. Wakati wa wiki hiyo iliyofanyika mkoani S  imiyu, Umoja wa Mataifa ulitumia fursa kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hasa ni kwa jinsi gani vijana wanaweza kusongesha ajenda hiyo. Miongoni mwa washiriki alikuwa kijana Riula Daniel ambaye ameonyesha kiu yake ya kukataa umaskini na kutokomeza magonjwa kwa kubuni jinsi ya kuzalisha mende na funza kibiashara. Je anafanya nini?

Mabadiliko ya tabianchi yabadili mwelekeo wa ufugaji wa jamii ya wamasai

Jamii ya wamasai ambao tangu enzi na enzi yajulikana kwa maswala ya ufugaji wa asili, sasa inajumuisha utamaduni na teknolojia ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, miongoni mwa jamii hizo ni ya wamasai wa Longido, Tanzania ambao wanapata elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwenda sanjari na ufugaji na kilimo.

Elimu hiyo inajumuisha utabiri wa hali ya hewa, majanga na changamoto zingine za kiasili. Ungana na Flora Nducha kwa undani zaidi katika makala hii.

Changamoto zinazowakabili watoto wa kike Uganda zaangaziwa

Jumuiya ya kimataifa leo imeadhimisha siku ya mtoto wa kike, ambapo ustawi wa kundi hilo umetajwa kuwa muhimu wakati huu ambapo malengo ya maendeleo endelevu SDGs yakiwa dira ya dunia.

Nchini Uganda wasichana wa kike wanakabiliwa na changamoto kadhaa katika ustawi wao ili kuwa tegemezi kwa taifa. Ungana na John Kibego anayeangazia chnagamoto hizo katika makala ifuatayo.