Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna nuru gizani, elimu kwa wakimbizi kutoka DRC

Kuna nuru gizani, elimu kwa wakimbizi kutoka DRC

Pakua

Kawaida maisha ya ukimbizini yanakuwa ni ya dhiki na taabu za kila aina. Lakini inaweza kutokea mkimbizi akafaidika kwenye maisha hayo ya kuomba hifadhi kwa njia moja ama nyingine. Hali ndivyo ilivyo kwa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walioko katika kambi ya Bwagiriza eneo la Ruyigi mashariki mwa Burundi. Licha ya masahibu ya maisha wanayokumbana nayo, baadhi ya wakimbizi watu wazima ambao awali hawakupata fursa ya

kuelimika, wamekuwa wanachangamkia kujifunza kusoma na kuandika katika darasa la kambini. Mwandishi wetu wa Burundi Ramadhani KIBUGA ameshuhudia wakimbizi hao wanavyodiriki visomo na ungana naye kwenye makala hii.

Photo Credit
Wakimbizi wakiwa darasani.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/Ramadhani Kibuga)