Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Uchangiaji damu waendelea New York

Majuma mawili baada ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuchangia damu mnamo Juni 14, upimaji damu kwa hiari unaendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Joseph Msami wa idhaa hii amejitolea kuchangia damu, fuatana naye katika safari yake kuanzia ofisini hadi katika eneo maalum la kuetekeleza kitendo hicho inachopigiwa chepuo na shIrika la afya ulimwenguni WHO.

Machafuko mapya Sudan Kusini, UNMISS yahifadhi raia zaidi

Kuzuka kwa machafuko nchini Sudan Kusini mwishoni mwa juma lililopita kumelazimisha vituo vya kuhifadhi wakimbizi wa ndani nchini humo vilivyo chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMSS kujiongeza na kuwahifadhi raia waiso na hatia.

Makala ifuatayo imegubikwa na simulizi za kusikitisha za madhila ya wakimbizi hao ambao sasa mustakabali wao umetatizika. Ungana na Joseph Msami

Wakimbizi wanapatiwa taarifa kuhusu hali ilivyo Somalia kabla ya kufanya maamuzi

Nchini Kenya harakati zinaendelea kuwawezesha wakimbizi 320,000 kutoka Somalia walioko kambi ya Dadaab kurejea nyumbani. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR ambalo ni moja wa pande tatu za kamisheni ya kuwarejesha kwa hiari wakimbizi waSomali kutoka Kenya.

Pande tatu hizo ikiwemo serikali ya Kenya, ile ya Somalia na UNHCR, wamefanya mazungumzo kwa lengo la kuona kwamba wakimbizi 150,000 wanarejea Somalia kwa hiari na kwa njia yenye hadhi na katika mazingira salama mwaka huu wa 2016.

Upimaji wa kiwango cha uchafuzi wa hewa ni muhimu katika kuzuia madhara- Muthama

Takriban watu bilioni tatu wanatumia mafuta yanayochafua mazingira lakini, Ushelisheli waliweza kuimarisha ubora wa hewa ndani ya makazi kwa kubadilisha matumizi ya majiko ya mkaa hadi majiko yaliyo rafiki kwa mazingira.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira, UNEP ambayo inataja hewa chafu kama muuaji wa kimya kimya. Aidha ripoti inasema kwamba nchi nyingi katika bara la Afrika hazijaweka viwango vya ubora wa hewa huku madhara yake yakitajwa kama mauaji ya wengi.

UN Photo/Shima Roy

Uharibifu wa vyanzo vya maji unazidi kuchochea uhaba wa bidhaa hii Karagwe, Tanzania

Upatikanaji wa maji katika nchi nyingi barani Afrika unakabiliwa na changamoto nyingi huku mchango wa bindamu na hata mabadiliko ya tabianchi vikiathiri hali hii.

Maji licha ya kwamba ni huduma ya msingi lakini watu wengi hawana uwezo wa kupata bidhaa hii na miongoni mwa sababu ni uharibifu wa vyanzo vya maji. Katika makala hii Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe Fm ya Kagera Tanzania anatupeleka Karagwe kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu uhifadhi wa vyanzo vya maji nchini humo, ungana naye.

Nilipata ulemavu wa kutoona nikiwa na umri wa miaka 16-Dkt. Kabue

Mkutano wa kikao cha tisa cha kamati ya mkataba kuhusu haki za watu wenye ulemavu, CRPD umekamilika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kikao cha mwaka huu kilikuwa na msisitizo wa kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanajumuishwa pia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma.

Ni jukumu la kila mmoja katika jamii kuhakikisha SDGs na ajenda ya Afrika ya 2063 vinafikiwa: TZ

Warsha ya siku mbili kuhusu masuala ya maendeleo endelevu yaani SDG’s na ajenda ya Afrika ya maendeleo yam waka 2063, imekamilika leo mjini Johanesburg Afrika ya Kusini.

Warsha hiyo iliandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP na serikali ya Kazakhstan.

Washiriki kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika yametuma wawakilishi kwenye warsha hiyo. Tanzania haikusalia nyuma iliwakilishwa na naibu katibu mkuu wizara ya fedha na mipango Amina Shaaban. Amezungumza na Flora Nducha wa

Idhaa hii na kuanza kumueleza Umuhimu wa warsha hiyo

Hamasa ya uchangiaji wa damu Uganda inahitajika zaidi.

Siku ya kimataifa ya kuchangia damu ikiadhimishwa hii leo Juni 14 kwa kauli mbiu changia damu okoa maisha, nchini Uganda akiba na hamasa ya uchangiaji wa damu ni suala linalohitaji hatua ya ziada. Baadhi ya wananchi wanafahamu umuhimu lakini wengine bado ni tatizo. Je nini kinafanyika? Ungana na John Kibego kwenye makala kutoka nchini humo itakayokupa kwa undani zaidi wa tukio hili