Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Fahamu utamaduni wa dansi India

Utamaduni ni maisha, ndivyo unavyoweza kusema ukiwa unatafakari na kuzingatia uatamaduni wa watu wa India ambapo pamoja na mambo mengine utamaduni wa jamii moja ya watu wa India ambao hucheza na nyoka huwashangaza wengi. Shirika la Umoja la Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO linapigia chepuo utamduni huu ambao uko hatarini kutoweka.

Ungana na Amina Hassan katika makala itakayopeleka nchini India huku pia ukijifunza utamaduni jadilifu wa nchi hiyo.

Nishati mbadala nchini Uganda

Upatikanaji wa nishati kwa wote ni changamoto kwa karne ya 21, wakati ambapo mtu mmoja kati ya watano hawapati huduma za umeme duniani, na Umoja wa Mataifa ukitarajia kuwa mahitaji ya nishati yataongezeka kwa asilimia 33 ifikapo mwaka 2035.

Miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs yaliyopitishwa mwaka 2015, lengo namba 7 ni kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu kwa wote na kwa bei nafuu.

Mwelekeo wa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania watia matumaini- UNFPA

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango imeonyesha ongezeko katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania. Takwimu zinasema kuwa matumizi sasa ni asilimia 27 ya watanzania wenye uwezo wa kutumia njia hizo ikiwemo sindano, vipandikizi na mipira ya kiume na ya kike.

Lakini ni hatua gani ambazo zimechangia ongezeko hilo japo linaelezwa kuwa ni la wastani? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Felister Bwana, Afisa programu wa afya ya mama na mtoto kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu, UNFPA nchini humo.

Mwelekeo wa uwekezaji wa kigeni Afrika watia shaka 2016- UNCTAD

Ripoti mpya ya kamati ya maendeleo ya biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kuhusu mwelekeo wa uwekezaji wa vitegauchumi wa kigeni duniani imeonyesha bayana kuzidi kudidimia kwa uwekezaji huo katika nchi za Afrika hususan zile zinazoendelea. Hata hivyo mataifa mengine yamenufaika kwa kupata uwekezaji mkubwa ambapo kwa ujumla yaelezwa kuwa uwekezaji huo duniani umeongezeka kwa asilimia 36 mwaka 2015. Je kwa ni nchi zipi zimenufaika zaidi? Sababu ni nini? Na mwelekeo ni upi unatarajiwa? Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt.

Usalama wa chakula CAR shakani

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati machafuko yamesababisha hali tete ya usalama wa chakula na hivyo kuongeza kadhia kwa raia wa nchi hiyo mjini na vijijini.

Watoto wanakumbwa na hatari ya utampiamlo huku afya ya jamii kwa ujumla ikizorota. Ungana na Grace Kaneiya katika makala inayofafanua madhila hayo na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kutoa usaidizi.

Picha: World Bank/Curt Carnemark

Kutoka Abu Dhabi hadi Afrika - matumizi ya nishati mbadala

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya nishati mapema wiki hii wamekuwa na mkutano mjini Abu Dhabi, falme za kiarabu kuhusu nishati za baadaye. Huu ni mkutano wa siku tano uliowakutanisha viongozi na wataalamu wa nishati endelevu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au ajenda 2030 wakati wa maadhimisho ya wiki ya uendelevu ya Abu Dhabi, au Abu Dhabi Sustainable Week.

Viongozi wanapaswa kutekeleza kwa vitendo dhamira yao ili kufankisha maendeleo Afrika-Kituyi

Kwa miongo minne sasa, mkutano wa jukwaa la uchumi limekuwa na lengo la kuimarisha hali kote ulimwenguni kitu ambacho kimesaidia katika programu ya mikutano ya kila mwaka.

Mkutano huo wa kila mwaka wa Davos, Uswisi ni moja ya kiungo muhimu kinachowakutanisha viongozi mbali mbali kwa ajili ya juhudi za pamoja zinazolenga kuimarisha malengo na ajenda ya viwanda duniani.

Wakati huu kunakoshuhudiwa teknolojia mpya zinazobadilisha jamii na hata uchumi viongozi wanahitajika kubadilishana mawazo kwa ajili ya mustakabali wao na kujiandaa na maisha ya baadaye.

Wananchi wa Sudan Kusini wamechoka kuwa tegemezi- Mogae

Hivi karibuni, Festus Mogae ambaye ni mwenyekiti wa kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini, JMEC, alikuwa ziarani kwenye maeneo ya Malakal na Bentiu. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kumwezesha kukutana na pande mbali mbali ikiwemo serikali, pande kinzani na hata mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu. Ziara ya Mogae ambaye pia ni rais wa zamani wa Botswana, ilianzia Malakal na hatimaye Bentiu, je alishuhudia nini? Grace Kaneiya anafafanua kwenye makala hii.

Matumizi ya dawa za kulevya na athari zake nchini Uganda

Matumiz ya madawa ya kulevya huwa ni kikwazo cha maendeleo ya jamii katika nchi nyingi duniani, na pia huhusishwa na utendaji wa makosa ya jinai. Nchini Uganda hasa kwenye Ziwa Albert, matumizi ya madawa hayo miongoni mwa vijana yanaarifiwa kuchochea uhalifu wa aina mbalimbali ukiwemo wizi, kama anavyosimulia John Kibego katika makala ifuatayo.

(Makala ya Kibego)

Idadi ya raia wa Msumbiji wanaowasili Malawi inaongezeka :UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi ya watu wanaokimbia Msumbiji na kutafuta hifadhi nchini Malawi imeongezeka sana katika wiki chache zilizopita.

Katika kijiji cha Kapise, wilaya ya Mwanza kilometa chache kutoka mji mkuu Lilongwe , timu ya UNHCR imeorodhesha watu  1,297 waliowasili huku theluthi mbili wakiwa wanawake na watoto na watu wengine Zaidi ya 900 wanasubiri kusajiliwa.