Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mustakhbali wa Burundi na DRC uko mikononi mwa jumuiya ya kimataifa:

Mustakhbali wa kijamii na kisiasa kwa mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Burundi kwenye ukanda wa maziwa makuu, uko mikononi mwa nchi husika na wadau wote wa ukanda mzima, Jumuiya ya Afrika Mashariki na jumuiya ya kimataifa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa mkutano wa kiamatifa kuhsu eneo la Maziwa Makuu, Zachary Muburi-Muita alipozungumza na idhaa ya Kiswahi ya Radio ya Umoja wa Mataifa.

Changamoto ya magonjwa ya moyo

Tarehe 29 Septemba kila mwaka dunia huadhimisha siku ya moyo. Siku ambayo wadau wa masuala ya afya wakiratibiwa na shirika la afya ulimwenguni WHO hutumia kama jukwaa la kuhamasisha kuhusu magonjwa ya moyo.

Ujumbe wa maadhimisho ya mwaka huu unalenga katika elimu kwa umma kwamba MOYO ni kitovu cha kila kitu yaani afya ambayo ndiyo uzima wa mwanadamu. WHO inataka jamii ifahamu kuwa moyo ukipata matunzo muruwa afya huwa sawia.

Mtu akipatiwa fursa lazima atabadilika - Assaf

Mwimbaji nyota wa kipalestina, Mohamed Assaf ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA. Yeye hutumia kipaji chake cha kuimba ili kuinua matumaini miongoni mwa wale ambao hata leo yao ni ndoto, sembuse kesho. Assaf alifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa tumbuizo maalum na ndipo alipofunguka kuhusu nyimbo zake na nafasi yake katika kuleta nuru kama inavyoelezea makala hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi.

Rushwa Tanzania ilishapevuka, sasa tunachukua hatua- Tanzania

Jumatatu ya Septemba 26, Tanzania iliwasilisha hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao cha mjadala mkuu wa wazi ambao hufanyika kila Septemba, mkutano wa baraza hilo unapoanza rasmi. Dkt. Augustine Mahiga ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki aliwasilisha hotuba iliyogusa masuala ya yanayogusa misingi ya Umoja wa Mataifa ambayo ni amani, usalama, maendeleo na haki za binadamu.

UN Photo/Loey Felipe

Idadi iongezwe na usawa uweko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa -Kenya

Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya Willam Ruto aliyeongoza ujumbe wa nchi yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kusaidia nchi zilizo na wahamiaji wengi. Akihojiwa na Rosemary Musumba wa idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa Bwana Ruto aligusia pia masuala ya usalama na misimamo mikali akisema hatua zichukuliwe ili kuepusha vijana kujitumbukiza kwenye ugaidi na hapa anaanza kwa kueleza juu ya wahamiaji ....

(Mahojiano na Ruto)

Msumbiji imepiga hatua kubwa katika kutunza mazingira

Serikali ya Msumbiji imepiga hatua kubwa katika kulinda mazingira , hali iliyoifanya kutunukiwa tuzo wiki hii hapa Marekani.

Hata hivyo kwa mujibu wa Rais wa nchi hiyo Fellipe Nyusi alipohojiwa na Flora Nducha wa Idhaa hii amesema wana mikakati kabambe ya utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi na waridhia mkataba huo hivi karibuni.

Lakini kwanza anafafanua juhudi zao za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s.

(MAHOJIANO NA RAIS FELLIPE NYUSI)

Kutambua mchango wa wakimbizi na wahamiaji ni muhimu sana-Somalia

Somalia inasema wakimbizi na wahamiaji wana mchango mkubwa katika jamii watokazo na waendako, tofauti na fikra za wengi kwamba watu hao ni chanzo cha madhila hasa kwa jamii zinazowapokea.

Hayo ni kwa mujibu wa mshauri wa kitaifa wa Somalia kuhusu masuala ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani, Bwana Ahmed said Farah, aliyeiwakilisha nchi yake katika mjadala wa ngazi ya juu kuhusu wakimbizi na wahamiaji Jumatatu.

Uganda ni mfano kwa usaidizi kwa wakimbizi #UN4RefugeesMigrants

Mkutano kuhusu wakimbizi na wahamiaji utafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa tarehe 19 mwezi huu. Lengo ni kuangazia ni mikakati gani ichukuliwe ili madhila ya wakimbizi yaweze kushughulikiwa kule waliko na hatimaye amani irejee makwao na hivyo waweze kurejea nyumbani.

Uganda imepokea wakimbizi zaidi ya 300,000 kutoka Sudan kusini, Burundi na DR Congo. Miongoni mwao,  200,000 wametoka Sudan Kusini. Licha mzigo huo wa wakimbizi, Uganda imetajwa kuwa ni nchi ambayo kwayo  hatua zake za usaidizi kwa wakimbizi zimekuwa ni mfano wa kuigwa. Je nini wamefanya?

Wanaume huona aibu kwenda ngumbaru- Tanzania

Nchini Tanzania ni asilimia 77 tu ya watu wazima na vijana ndio wanajua kusoma na kuandika hiyo ni kwa mujibu wa Baselina Levira, Mkurugenzi msaidizi, Elimu ya watu wazima na elimu njia ya mfumo rasmi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alipohojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania. Bi. Levira alitoa takwimu hizo wakati wa siku ya kisomo duniani ambapo alisema kiwango hicho ni cha chini ikilinganishwa na miaka ya themanini ambapo ni asilimia Tisa nukta Sita tu ya watanzania ndio walikuwa hawajui kusoma na kuandika.