Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Kampuni za sigara haziogopi kusema uongo- Dkt. Ouma

Je umewahi kujiuliza kwa nini paketi za sigara na bidhaa za tumbaku au matangazo ya bidhaa hizo yana picha na rangi za kuvutia? Shirika la afya ulimwenguni, WHO linasema hiyo ni kampeni ya kampuni za sigara za kuhakikisha kuwa zinaweza rangi na vivutio hata kutumia watu mashuhuri ili kuhakikisha wavutaji wawe wakubwa au wadogo wananasa kwenye mtego wa uvutaji bidhaa hiyo yenye hatari kubwa kwa afya. Sasa leo ikiwa siku ya kutotumia bidhaa za tumbaku, WHO imekuja na maudhui mahsusi ya kuwa na vifungashio visivyo na alama au rangi yoyote na sababu ni nini? Anafafanua hapa Dkt.

#WHS: Wanawake wapewe kipaumbele katika kushughukilia masuala ya kibinadamu

Kila kunapozuka dharura katika jamii waathirika wakubwa ni wanawake ingawa jamii nzima inaathirika. Hivyo wito umetolewa wa kuwapa kipaumbele wanawake hasa zahma za kijamii zinapotokea.

Wito huo umetolewa na mwakilishi wa vijana wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya Hanna Wanja Maina akiwa mjini Istanbul Uturiki wakati wa hitimisho la mkutano wa dunia wa masuala ya kibinadamu alipozungumza na Radio ya Umoja wa mataifa

(HANNA 1).

Hanna anaeleza pia nini amejifunza kwenye kongamano hilo la kimataifa

(HANNA 2)

Mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji ni kipaumbele chetu: Mwenengabo.

‘‘Tunawasidia wakimbizi na wahamiaji kisaikolojia na kiafya ili kuwapa unafuu wa kimaisha’’ amesema Mkurugenzi wa taasisi ya haki za watu wa asili Afrika Mashariki na kati ECAAIR Fredrick Mwenengabo.

Katika mhojiano na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa Mwenengabo ambaye alihudhuria mkutano wa jamii asilia mjini New York anasema amekutana na wadau wa masuala ya wakimbizi na kibinadamu ili kupata usaidizi zaidi.

Awali anaeleza ujumbe wake katika mkutano uliomalizika wa jamii asilia.

(SAUTIMAHOJIANO)

Operesheni zetu Beni zinazaa matunda dhidi ya ADF- Meja Kahoko

Siku ya kimataifa ya ulinzi wa amani huadhimishwa tarehe 29 mwezi Mei ya kila mwaka ikilenga kukumbuka walinda amani waliopoteza maisha yao kuhakikisha amani inakuwepo duniani, lakini vilevile kuangazia wanawake na wanaume ambao wamesafiri mbali na makwao ili kutekeleza jukumu hilo adhimu.

Hii leo tunamuangazia Meja Francis Anatory Kahoko, Naibu afisa usalama kwenye kikosi cha FIB ambacho ni cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO.

Sarakasi yaleta vijana wa mataifa mbalimbali Afrika

Sanaa ni moja ya njia za kuunganisha watu wa jamii au hata mataifa tofauti. Aina mbali mbali za sanaa huwaleta watu pamoja na kusahau tofauti zao na hata kujenga mustakhbali wao. Miongoni mwa sanaa ni sarakasi ambayo ilikutanisha zaidi ya wanasarakasi 100 huko Ethiopia wakiangalia jinsi ya kuimarisha kazi zao na wakati huo huo kutoa burudani. Je nini kilifanyika? Ambatana na Joshua Mmali katika makala hii.

Ukuaji wa miji ni muhimu uende sambamba na SDGs:UN-HABITAT

Ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa makazi UN-HABITAT iliyozinduliwa leo, inasema ukuaji wa miji ni jambo ambalo litaendelea lakini ni vyema ukaenda sambamba na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs.

Ripoti inasema ifikapo mwaka 2030 zaidi ya nusu ya watu wote duniani watakuwa wanaishi mijini, na ili kukidhi mahitaji yao serikali lazima zianze sasa kuweka mipango kabambe. Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii kuhusu ripoti hiyo, Tom Osanjo, mwandishi na afisa mawasiliano wa UN-HABITAT anaanza kwa kufafanua yaliyogusiwa ndani ya ripoti hiyo.

Picha:UM/Rick Bajornas

Jamii asilia zatangaza utamaduni wake New York

Mkutano wa 15 wa jamii ya watu wa asili unaendelea hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, jamii hiyo pamoja na kujadili mambo kadhaa yahusuyo utatuzi wa migogoro na amani, pia inatangaza utaamaduni wake kwa dunia.

Joseph Msami amefuatilia muziki wa asili wa jamii hiyo wakati wa mkutano huo. Ungana naye katika makala itakayokueleza kinagaubaga utamaduni wa jamii asilia.

Nchini DRC, watu wa asili waendelea kunyanyaswa

Haki za watu wa jamii za asili bado hazitambuliwi ipasavyo, amesema mmoja wa wawakilishi wanaohudhuria mkutano wa 15 wa mjadala wa kudumu wa watu wa asili unaofanyika mjini New York Marekani.

Mochire Diel ni mwakilishi wa watu wa jamii ya Bambuti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambao kwa mujibu wake idadi yao nchini humo ni takriban 750,000.