Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mradi wa pamoja waleta nuru vita dhidi ya GBV-Kenya

Nchini Kenya wadau mbali mbali wanashirikiana katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia, GBV kupitia programu ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake Jowege.

Programu ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya. Lengo la programu hiyo ni kuimarisha uwezo wa wahusika ili kuweza kukabiliana na kuzuia ukatili wa kijinsia.

Jamii ya Bambuti yategemea kurejeshwa kwa uhifadhi wa Okapi DRC

Msitu wa Epulu ambao umeorodheshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni UNESCO kama urithi wa dunia umesheheni bayoanuai.

Miongoni mwa maajabu yanayopatikana kwenye msitu huu pekee duniani kote ni aina ya mnyama adimu sana, aitwaye Okapi.

Msitu huo pia ni makazi ya jamii ya watu wa asili wa Pygmee wanaofahamika kama Bambuti, ambao maisha yao yalikuwa yanategemea wanyama pori. Lakini maisha hayo sasa yako hatarini.

Tutawainua wasichana kiuchumi: Jesca Mmari

Tutajengea uwezo wa wanawake na wasichana na kuwajumuisha wanaume , amesema Jesca Mmari ambaye ni mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake wa taasisi ya wasichana wakristo Tanzania YWCA.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii baada ya kuhudhuria mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW uliomalizika mwishoni mwa juma lililopita, Jesca anaanza kuzungumzuia umuhimu wa maazimio yaliyofikiwa

(SAUTI MAHOJIANO)

Pazia zafungwa, mkutano wa CSW60 jijini New York

Mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanwake CSW60 umefunga pazia makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. Wanawake wawakilishi wa serikali na mashirika mbalimbali wamejadili kuhusu masula nyeti ya ustawi wao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika kufikia malengo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Je nini kilijiri katika mkutano huo wa wiki mbili? Joshua Mmali anasimulia zaidi…

(Studio pkg)

Mtaala wa ukatili dhidi ya wanawake waleta mabadiliko Kenya: Veronica

Mbinu ya mtaala wa ukatili dhidi ya wanawake imeleta mabadiliko makubwa nchini Kenya amesema Veronica Shiroya kutoka taasisi ya kimataifa ya miongozo kwa wasichana WAGGSS nchini humo.

Katika mahojiano na Joseph Msami baada ya kuhutubia moja ya mikutano iliyoangazia ukatili wa kijinsia wakati wa mkutano wa 60 wa kamisheni ya wanawake CSW60 uliokamilika mjini New York, Veronica anaaza kuelezea kinagaubaga mbinu hiyo na kisha matokeo yake.

(SAUTI MAHOJIANO)

Hakuna lisilowezekana, Libya itafikia mwafaka: Kikwete

Licha ya kwamba taifa limegawanyika kutokana na kuwa na mamlaka nyingi zinaozoongoza, bado kuna matuamaini ya suluhu Libya amesema Mjumbe maalum wa Muungano wa Afrika AU katika mzozo wa Libya Jakaya Kiwete.

Katika mahojiano maalum kwa njia ya simu kutoka Tunisia kulikofanyika mkutano wa kusaka suluhu la kisiasa, Kikwete ambaye pia ni Rais mstaafu wa Tanzania amemueleza Joseph Msami kuwa ameanza hatua za awali za kujifunza kinachotatiza Libya.

( SAUTI MAHOJIANO)

Muarubaini wa suluhu ya Burundi ni makubaliano ya Arusha: Balozi Manongi

Suluhu la mgogoro wa kisiasa nchini Burundi lazima litokane na misingi ya makubaliano  ya Arusha  ambayo ilizaa matumaini kwa taifa hilo la Afrika Mashariki,  amesema mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York Balozi Tuvako Manongi.

Katika mahojiano na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kulihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi Manongi anaanza kuelezea ujumbe aliouwasilisha kwenye baraza hilo lililojadili hali ya amani na usalama nchini Burundi.

Wanawake wakiwezeshwa na kuendelea, na nchi inaendelea- Josee Ntabahungu

Wiki ya kwanza ya kikao cha 60 cha Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake (CSW60) imehitimishwa hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani, kikao hicho kikiwa kimewaleta pamoja wanawake na wanaharakati wa haki za wanawake kutoka kote duniani.

Mmoja wa washiriki kutoka Afrika Mashariki, ni Josee Ntabahungu, Meneja wa Programu ya Kuendeleza Wanawake katika Shirika la Care International, nchini Burundi.

Wabunge vijana walenga kumaliza ufisadi na kuimarisha uwazi

Zaidi ya wabunge vijana 130 kutoka mabunge mbalimbali dunia wameelezea utayari wao wa kuimarisha uwazi na usimamizi wa fedha za umma kama msingi wa kukabiliana na ufisadi baada ya kuhitimisha mkutano wa siku mbili katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Wabunge hao ambao walihudhuria kongamano la tatu la vijana wabunge la Muungano wa wabunge duniani, IPU #youngMPs wamefikia makubaliano hayo ya kuimarisha uchunguzi katika bajeti ya taifa kama moja ya mikakati ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs kufikia mwaka 2030.

UN Photo/Evan Schneider

Ujasiriamali wamkomboa mwanamke Tanzania

Uwezeshaji wa wanawake kupitia ujasiriamali ni mbinu mojawapo ya kuinua wanawake kiuchumi. Martin Nyoni wa redio washirika redio SAUT ya Mwanza Tanzania amefanya mahojiano na mmoja wa wanawake waliojikomboa kiuchumi kwa kupitia mgahawa wa chakula.