Homa ya ini bado ni changamoto Uganda
Tarehe ishirini na nane Julai kila mwaka dunia huadhimisha siku ya homa ya ini. Shirika la afya ulimwenguni WHO huitumia siku hiyo kuhamasisha makabiliano dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Katika maadhimisho ya mwaka huu, WHO inazitaka nchi wanachama kuchukua hatua haraka kuboresha ufahamu kuhusu homa ya ini, kuongeza fursa ya kufanyiwa vipimo na kupata huduma ya tiba.
Duniani kote watu milioni 40 wameambukizwa homa ya ini aina B na C, ikiwa ni mara 10 zaidi ya watu wanaoishi na VVU.