Ugonjwa wa malaria na juhudi za kuutokomeza Tanzania
Tarehe 25 mwezi Aprili ya kila mwaka, dunia huadhimisha siku ya malaria, msisistizo ukiwa kutokomeza ugonjwa huo. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya ulimwenguniWHO, takribani watu bilioni 3.2 ambayo ni karibu nusu ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kuambikizwa malaria.
Mwaka 2015 visa zaidi ya milioni 200 vya malaria viliripotiwa na zaidi ya vifo Laki Nne. Bara la Afrika hususani nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinabeba mzigo mkubwa ambapo WHO inasema kwamba mwaka 2015 bara hilo lilikuwa na asilimia 89 ya visa vya malaria na asilimia 91 ya vifo.