Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Ajali ya barabarani hukwamisha uwezo wa manusura wa ajali

Ripoti ya hali ya usalama barabarani ya mwaka 2015 ikiangazia mataifa 180 inasema kwamba idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani imeongezela huku maafa mengi yakishuhudiwa nchi za kipato cha chini.

Kutokana na hali hiyo, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita mataifa yalipanga sheria angalau moja kuambatana na sheria za barabarani ikiwemo: kufunga mkanda, dereva kutotumia mihadarati na kuzingatia mwendo kasi.

Umuhimu wa vyoo na huduma za kujisafi

Nyumba ni choo! Huu ni usemi ambao hutumika mara nyingi ukiangazia umuhimu wa choo bora na huduma za kujisafi nyumbani.

Tarehe 19 mwezi huu ilikuwa ni siku ya choo duniani.  Dunia imekumbushwa kuwa choo na huduma za kujisafi ambazo hazipewi umuhimu zaweza kuchangia ukuaji wa uchumi.

Umoja wa Mataifa katika taarifa yake umesema maadhimisho ya mwaka huu yana maudhui ya vyoo na ajira na umuhimu wa huduma za kujisafi au ukosefu wake katika ustawi na mazingira ya kazi.

Muziki waelimisha kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake, sambamba na siku 16 za harakati dhidi ya vitendo hivyo kote duniani, ujumbe wa utokomezaji unafikishwa kwa njia mbalimbali.

Njia mojawapo ni muziki ambapo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumegfanyika tukio maalumn lililowakusanya wadau wa harakati za ukatili dhidi ya wanawake. Burudani ilitamalaki ikienda sanjari na ujumbe. Amina Hassan anasimulia katika makala ifuayato.

UN Photo/Logan Abassi

Bila viwanda hakuna maendeleo endelevu Uganda

Umoja wa Mataifa unasema maendeleo endelevu barani Afrika yanahitaji viwanda ambavyo vitakuza ajira maradufu katika bara hilo ambalo kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita uchumi wake umekua kwa zaidi ya asilimia nne.

Nchini Uganda kama zilizvyopnchi nyingi, umuhimu wa viwanda kwa maendeleo ya taifa hilo hauna mjadala. Ungana na John Kibego anayemulika ajira kupitia viwanda Uganda.

Muziki unaleta pamoja itikadi, dini na imani tofauti: Sheilla

Kutana na Sheilla Akwara, mwanamuziki kutoka Kenya anayeng’ara katika muziki wa injili.

Mwanamuziki huyu ambaye amekuwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kwa miezi kadhaa akifanya mafunzo ya kazi, anatumia muziki wake kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali ikiwamo amani na utengamano. Fuatana na Joseph Msami katika makala inayomulika kipaji cha Sheilla .

Kazi na dawa, taswira Marrakesh, #COP22

Mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP22 unaendelea huko Marrakesh, Morocco. Mkutano huu unajadili mada tofauti kwa ajili ya kuwezesha jamii na serikali kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi sanjari na kufanikisha kutekeleza mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka jana. Kando na mada zikiangazia maswala hayo muhimu, wakazi wa Marrakesh waliandaa tumbuizo, yaani kazi na dawa. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii kufahamu walifanya nini.

Kilimo cha kisasa na chenye tija miongoni mwa wakulima nchini Uganda

Wakati mkutano wa 22 nchi  wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi ukiendelea mjini Marrakesh nchini Morocco, moja ya mada zinazojadiliwa ni kilimo endelevu , chenye tija na na ambacho kinahifadhi mazingira.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiongozwa na lile la chakula na kilimo FAO yameeleza umuhimu wa kilimo hai katika kupunguza uharibifu wa mazingira, ikielezwa kuwa shughuli za kilimo zinaathiri mazingira. Uharibifu huo ni kupitia matumzi holela ya ardhi, mbolea ya samadi n ahata za kawaida hutoa gesi chafuzi zinazokwangua ukanda wa ozone.