Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Elimu jumuishi yakwamua watoto Burundi

Watu wenye ulemavu ni kundi lililo hatarini zaidi kubaguliwa katika nyanja mbali mbali kama elimu, afya na huduma za kijamii kwa ujumla, Moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ni kuhakisha maslahi ya watu walemavu yanazingatiwa kwa kuwajumusha katika masuala yanayowahusu zaidi. Moja ya mambo yanayopigiwa chepuo ni elimu jumuishi kwa watu walemavu na mwenzetu Ramadhan Kibuga anatupeleka Burundi katika makala ifuatayo kufahamu zaidi..

Mcheza piano atumia kipaji chake kuleta nuru kwa watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF huchagua watu mashuhuri au wenye ushawishi miongoni mwa jamii kuliwakilisha na kueneza ujumbe wake a haki na elimu kwa waototo duniani. Mmoja wao aliyeteuliwa hivi karibuni ni raia wa nchi ya Jordan ambaye pia ni mcheza piano mashuhuri Zade Dirani.

Je anafanya nini kuleta nuru kwa jamii zilizogubikwa na huzuni na machungu? Ungana basi na Brian Lehander kwenye makala hii kwa maelezo zaidi..

Siku ya usaidizi wa kibinadamu twaelekea Bugambe, Uganda

Kila Agosti 19, dunia huadhimisha siku ya usaidizi wa kibinadamu ambapo mwaka huu maudhui ya siku hii ambayo lengo lake ni kuthamini mchango wa watu wanaotoa usaidizi wa kiutu pamoja na kuwakumbuka wale waliopoteza maisha yao wakati wa kutimiza wajibu huo ni utu wa pamoja. Tunaangazia kilichofanyika makao makuu ya umoja huo New York, Marekani na pia tutaungana na mwenzetu John Kibego aliyetembelea wakimbizi huko Uganda.

Mwanamuziki mwenye ulemavu wa kutoona anga’ra kimataifa

Kuwa mlemavu wa kutoona hakukumzuia kabisa mwanamuziki chipukizi kutoka Nigeria Cobhams Asuquo kushamiri hadi ngazi ya kimataifa.

Hii ni sehemu ya simulizi ya kusisimua katika makala iliyoandaliwa na Joseph Msami ambayo inaangazia juhudi za Shirika la Kimataifa la Haki Miliki WIPO kulinda na kuhifadhi haki za wabunifu, na wenye vipaji mbalimbali wakiwamo waimbaji.

Marimba ya Afrika yameota mizizi Colombia

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linapigia chepuo utamaduni wa nyimbo kama sehemu ya kutunza urithi wa dunia katika mila na tamaduni mbali mbali. Muziki unaotumia ala za marimba ambao ni alama ya utamaduni wa watu wenye asili ya Afrika walioko maeneo mbali mbali duniani ikiwemo Ecuador na Colombia ni moja ya vitu ambavyo UNESCO inataka kuhifadhi. Joseph Msami katika makala ifuatayo anasimulia jinsi muziki huo unavyotumika kuhifadhi historia na hadhi ya watu hao wenye asili ya Afrika huko Colombia.

Nishati mbadala yabadilisha maisha ya jamii Uganda

Nchini Uganda wananchi wanatumia mbinu mbadala ya nishati kuendesha shughuli zao za kila siku na pia kupata kipato. Mbinu hizi ni moja ya juhudi za kupambana na umasikini na pia kulinda mazingira ikiwa ni baadhi ya malengo ya maendeleo endelevu.

Basi tuungane na John Kibego katika makala hii kufahamu zaidi.

Unyonyeshaji mtoto uanze saa moja tu baada ya mtoto kuzaliwa

Tarehe Mosi hadi Saba Agosti ya kila mwaka ni wiki ya Unyonyeshaji, siku ambayo Umoja wa Mataifa imetenga kuangazia jambo hili adhimu kwa makuzi ya mtoto na kwa mustakhbali wake wa baadaye. Shirika la afya duniani, WHO linasema kila mama mzazi anaweza kunyonyesha, alimradi apatiwe taarifa sahihi na jamii nayo imuunge mkono, sanjari na mfumo wa afya. Colostrum, ambayo ni maziwa yenye rangi ya manjano na mazito yatokayo pindi tu mama anapojifungua, yanaelezwa na WHO kuwa ni muhimu sana kwa mtoto aliyezaliwa na mama anapaswa kuanza kunyonyesha saa moja tu baada ya kujifungua.

Mwanamuziki kiziwi atumia muziki kupigania ujumuishwaji wa kijamii

Wakati mikutano ya mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha, IMF, mapema mwaka huu, palitokea mgeni mmoja aliyewashangaza wengi.

Signmark ni msanii wa muziki wa kufokafoka (au rap), kutoka Finland. lakini ajabu ilikuwa ni kwamba, yeye ni kiziwi. Wakati huo, alizungumzia jinsi alivyovunja sheria, kwa kuwa kiziwi wa kwanza kabisa kuwahi kupata mkataba wa kurekodi, na jinsi ambavyo amehamasisha umma kuhusu umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii.

Kufahamu zaidi, ungana na Joshua Mmali katika makala hii.

Joto kali lachangia ugumu wa maisha kambini

Maelfu ya wakimbizi kutoka Iraq wamesambaratishwa na vita, na wengi wao kuishia katika kambi mbali mbali zenye hali mbaya. Moja ya kambi hizo ni kambi iliyo ndani ya jangwa la Ameriyat al-Fallujah, huko nchini Iraq.

Katika makala hii tunakuletea madhila anayokumbana nayo mkimbizi mmoja na familia yake baada ya kufungasha virago kutokana na vita. Ungana na Joseph Msami kwa simulizi zaidi.