Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Wanawake wajikwamua kiuchumi Uganda

Kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake ambayo huadhimishwa kila Machi nane, ambapo utekelezaji wa melengo ya maendeleo endelevu SDGs kwa kuzingatia usawa wa kijinsia unamulikwa, nchini Uganda wanawake licha ya kukabiliana na utamaduni kinzani wanajikwamua kiuchumi.

Ungana na John Kibego katika makala inayomulika juhudi hizo zinazopigiwa chepuo na mamalaka za serikali.

Kenya imepiga hatua katika elimu, afya na upatikanaji wa maji safi- Ripoti

Wiki hii, Kenya imewasilisha ripoti yake huko Geneva, Uswisi, kuhusu hali ya haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni mbele ya kikao cha 57 cha kamati ya makubaliano ya kimataifa juu ya haki hizo.

Ripoti hiyo ambayo inaendana na ibara ya 16 ya makubaliano ya kiuchumi, kijamii na utamaduni ICESCR imetanabaisha hatua ambazo Kenya imepiga katika kufanikisha mapendekezo ya makubaliano hayo.

Kuzuru Afrika Mashariki kumemfanya msanii Drew Holcomb kuvalia njuga umaskini

Mwanamuziki wa Kimarekani Drew Holcomb, ni mmoja wa wasanii waliopata kushiriki katika mfululizo wa vipindi vya Benki ya Dunia, vya Muziki kwa Maendeleo. Baada ya kuzuru maeneo kadhaa ya Afrika Mashariki, msanii huyo kutoka mji wa Nashville, katika jimbo la Tennessee, Marekani, alitambua kuwa kuna uhaba mkubwa wa huduma za maji safi na huduma za kujisafi, pamoja na matatizo ya lishe duni miongoni mwa watoto. Tangu wakati huo, amekuwa akijihusisha na shughuli za mashirika ya kibinadamu, kama vile One Egg na Blood: Water, ili kusaidia kuleta huduma hizi kwa watu wanaozihitaji zaidi.

Kuondoa umaskini kupitia usawa wa kijinsia: Rwanda

Nchini Rwanda, zaidi ya familia 6,000 wamepatiwa mafunzo ya kuimarisha kipato chao na upatikanaji wa chakula kupitia mifugo.

Kwa mujibu wa Mfuko wa Kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD ambao umeshirikiana na serikali ya Rwanda katika mradi huo uitwao KWAMP, mafanikio zaidi yamepatikana kwa sababu mradi umehusisha mafunzo kuhusu usawa wa kijinsia.

Tayari Rwanda ikiongoza duniani kwa uwiano wa wanawake bungeni, sasa inategemea kukuza maendeleo kwa kuwapa wanawake nafasi zaidi katika maswala ya kiuchumi.

Lugha ya mama kama chombo cha kutoa mafunzo Afrika Mashariki

Februari 21 ni siku ya lugha ya mama duniani.Kauli mbiu ya mwaka huu ni:  “Elimu yenye ubora, lugha inayotumika kufundisha na matokeo yake.” Hii inasisitiza umuhimu wa lugha ya mama kwa ajili ya ubora wa elimu na katika uwepo wa lugha mbalimbali.

Katika ujumbe wake wa mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova amesema kwamba Lugha za mama katika muktadha wa lugha zaidi ya moja ni kiungo muhimu katika kuhakikisha elimu bora, ambayo  ni msingi wa kuwaimarisha wanawake na wanaume katika jamii.

Okestra kutoka Venezuela yapigia chepuo amani

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki hii kumefanyika tumbuizo la muziki kwa ajili ya kupigia chepuo amani. Amani japo ni neno lenye herufi tano, bado imesalia kuwa ndoto kwa wakazi wengi duniani wakati huu ambapo watu zaidi ya Milioni 123 wamefurushwa makwao kutokana na mizozo iwe ya kiasili au inayosababishwa na binadamu. Tamasha hilo lilihusisha okestra kutoka Venezuela na kwa yaliyojiri tuungane na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Kuna matumaini ya watoto wakimbizi kupata elimu licha ya hali ya ukimbizini

Nchini Ethiopia, idadi ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini ni zaidi ya 350,000. Miongoni mwao, Shirika la Umoja wa MAtaifa la Kuhudumia wakimbizi UNCHR linakadiria kwamba zaidi ya 100,000 ni watoto wenye umri wa kwenda shuleni. Lakini nusu yao tu wamejiandikisha shuleni.

Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kule ilioko nchini Ethiopia, mvulana mmoja ameshikilia majukumu katika kuwafundishia wenzake.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

Umoja wa Mataifa waanza kuondoka Liberia, amani yarejea

Kuna usemi usemao nyota njema huanza kuonekana asubuhi, usemi huu unaonekana kutimia katika taifa lililoko Afrika Magharibi Liberia,  ambalo baada ya kushuhudia vita ya wenyewe kwa wenyewe taifa hilo sasa linaelekea kwenye nuru.

Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake nchini humo UNMIL umejiandaa kuondoka nchini humo baada ya kuwezesha ulinzi wa amani hatua iliyoambatana na kusaidia vikosi vya usalama kuimarisha amani nchini humo. Ungana na Joseph Msami katika makala itakayokupa undani zaidi.

Redio yaelimisha jamii kuhusu malaria DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Radio washirika Umoja imejitahidi kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa malaria uliokithiri kwenye eneo la Fizi, Kivu Kusini.

Kupitia programu mbali mbali redio hiyo imetoa mafunzo kwa wananchi kuhusu jinsi ya kujikinga na mbu na kuzuia maambukizi ya malaria. Wasikilizaji wamenufaika na mafunzo hayo, kadhalika viongozi wa sekta ya afya hadi visa vya malaria vikaanza kupungua, hii kiwa ni ishara ya umuhimu wa redio katika kuokoa maisha wakati huu dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya redio hivi karibuni.

Redio ya Umoja wa Mataifa imechangia kukuza Kiswahili- Abdillahi Zuberi

Leo tarehe 13 Februari ni Siku ya Kimataifa ya Redio Duniani. Leo ni siku maalum pia, kwani Redio ya Umoja wa Mataifa inaadhimisha miaka 70 tangu azimio lililokianzisha chombo hicho adhimu cha kupasha habari na kubadilishana mawazo.

Redio ya Umoja wa Mataifa inatangaza kwa lugha nane, zikiwemo Kiswahili, Kireno na lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kirusi, Kichina na Kihispania.