Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Mbinu mpya za kilimo zaokoa wakulima Guatemala

Nchini Guatemala, ukame umekuwa mwiba kwa wakulima, kilimo chao kimekuwa cha mkwamo, wakiwaza kutwa kucha nini cha kufanya ili kunasua maisha  yao. Hata hivyo wataalamu wa kilimo wameibuka na mbinu ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabiachi, wakati huu ambapo mkataba wa mabadiliko ya tabianchi ukitaka wakulima nao wasaidiwe ili kilimo kiwe endelevu. Je ni kitu gani wanafanya? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Msalala yaonyesha njia katika ulinzi wa Albino Tanzania- UNESCO

Ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania umekuwa ni tatizo lililosababisha Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kuchukua hatua. Hatua hizo zilihusisha mikakati ya kijamii yenye lengo la kushirikisha viongozi, jamii na watoa huduma kwa kundi hilo ili kupunguza na hatimaye kutokomeza ukatili huo ambao kati yam waka  2000 na 2015 umeshuhudia zaidi ya mashambulio 150 nchini humo. Je ni nini kilifanyika? Mathias Herman Luhanya ni afisa programu kutoka UNESCO na amezungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii.

Ustawishaji wa miji Afrika Mashariki

“Miji inaendelea kuwa makazi ya binadamu na ni kiini cha vitendo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, ukuaji wa dunia, amani na haki za bindamu.” Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa siku ya miji duniani iliyoadhimishwa Oktoba 31 mwaka huu.

Yaelezwa kuwa ifiakapo mwaka 2050 idadi ya wakazi duniani itaongezeka kwa theluthi mbili.

Mwaka huu Umoja wa Mataifa umechagua kauli mbiu, “miji jumuishi, maendeleo kwa wote” kwa ajili ya kuhimiza mchango mkubwa wa ukuaji miji kama kitovu cha maendeleo ulimwenguni na ushrikishwaji wa jamii.

Vijana mjini Mogadishu wataka jiji lenye amani

Nchini Somalia, vurugu na ripoti za mapigano kila uchao huweka fikra ya kwamba hakuna maisha ya kawaida nchini humo. Fikra hizo zilizoota mizizi zimefanya vijana wa kisomali hususan kwenye mji mkuu Mogadishu kupaza sauti wakitaka harakati za kuchochea amani na ustawi wa kiuchumi kwa mustakhbali bora wa jiji lao. Vijana hao walipaza sauti zao kwenye kampeni iliyopatia maudhui, ‘Jiji tulitakalo” na Brian Lehander ni shuhuda wetu..

UN Photo/Sylvain Liecht

Nawindwa, sina uhuru: Mwanahabari Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la  Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO linasema kuwa wanahabari takribani 800 wameuawa katika kipindi cha muongo mmoja kote duniani.

Novemba mbili kila mwaka ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji sheria ya uhalifu dhidi ya waandishi wa habari, mwanahabari mmoja nchini Uganda amesimulia mikasa inayomkabili kwa kuwa ametekeleza wajibu wake.

Ungana na John Kibego katika makala ifuatayo.

Juhudi za kukabiliana na athari za tabianchi zinahitaji kupigwa jeki-Balozi Kamau

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kushuhudiwa katika mataifa mbali mbali yakiwemo mataifa ya bara la Afrika. Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi, Balozi Macharia Kamau ambaye alikuwa ziarani kushuhudia hali halisi ya athari za mabadiliko hayo kusini mwa Afrika amesema watu na wanyama wakufugwa na wale wa porini ni waathirika.

Mabadiliko ya tabianchi na ukosefu wa chakula Tanzania

Ukame ambao unatokana na mabadiliko ya tabianchi sasa ni dhahiri na athari kama vile ukosefu wa chakula, umeanza kuathiri nchi hususani barani Afrika.

Nchini Tanzania, mkoani Kagera, moja ya mikoa yenye historia ya kuwa na chakula kingi kutokana na ardhi yenye rutuba sasa imeanza kuathirika. Ungana na Tumaini Anatory wa redio washirika Karagwe Fm ya mkoani humo katika makala ifuayato.

Tanzania kunufaika na ushirikiano wa kikanda: Balozi Ali Siwa

Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ni lazima itegemee ushirikiano baina ya nchi wanachama wake wala si mashindano, wamesema washiriki wa mjadala wa kisiasa uliofanyika wiki hii mjini Kigali nchini Rwanda kuhusu ukhirikiano wa kikanda.

Kwa mujibu wa Kaimu mkuu wa ofisi ya Afrika Mashariki ya Kamisheni ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika, ECA, Andrew Mold, chumi zote za nchi za Afrika Mashariki zimenufaika na muungano wa kibiashara wa EAC, hasa Tanzania, ambapo takwimu zinaonyesha kwamba biashara yake ndani ya EAC imeongezeka mara tatu tangu mwaka 2011.

Wanawake Burundi na fursa za kuzalisha

Ulimwengu  huadhimisha tarehe 15 Oktoba  siku ya kimataifa ya Mwanamke wa kijijini. mwaka huu , siku hiyo imeangazia nafasi ya malengo ya maendeleo endelevu katika kuwawezesha wanawake wa mashinani na kuwajumuisha katika  kuongeza maradufu uzalishaji wa kilimo na  kipato cha wazalishaji wadogo wadogo.

Huko Burundi, wanawake wa Vijijini wamekuwa wanachangamkia kilimo kwa kujumuika kwenye mashirika, hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao.