Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Burundi na fursa za kuzalisha

Wanawake Burundi na fursa za kuzalisha

Pakua

Ulimwengu  huadhimisha tarehe 15 Oktoba  siku ya kimataifa ya Mwanamke wa kijijini. mwaka huu , siku hiyo imeangazia nafasi ya malengo ya maendeleo endelevu katika kuwawezesha wanawake wa mashinani na kuwajumuisha katika  kuongeza maradufu uzalishaji wa kilimo na  kipato cha wazalishaji wadogo wadogo.

Huko Burundi, wanawake wa Vijijini wamekuwa wanachangamkia kilimo kwa kujumuika kwenye mashirika, hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao.

Mwandishi wetu wa maziwa makuu, Ramadhani Kibuga ametembelea katika  mkoani Cibitoke eneo la Rugombo lililoko  kwenye mpaka wa Burundi na Rwanda na kushuhudia kasi ya kilimo cha kinamama  vijijini kwenye eneo hilo. Ungana nao.

Photo Credit
Wanawake wakulima nchini Burundi.(Picha:FAO)