Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

23 Februari 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tutakuletea mada kwa kina kutoka viziwani Zanzibar nchini Tanzania , ambapo ikiwa imesalia chini ya miaka 8 kufikia ukomo wa malengo ya amendeleo endelevu SDG’s juhudi zinafanyika kwa hali na mali kuhakikisha jamii zinafikia malengo hayo. Miongoni mwa wanaharakati wa kupigia upatu malengo hayo ni mke wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Bi. Mariam Mwinyi ambaye mwishoni mwa wiki amezindua wakfu au taasisi maalum ijulikanayo kama “Zanzibar Maisha Bora Foundation”.

Sauti
15'32"

22 Februari 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo miongoni mwa utakayosikiani pamoja na ziara ya Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC, kumuwakilisha Katibu Mkuu.

Naibu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Somalia, Adam Abdelmoula, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzisaidia haraka jamii zilizoathirika vibaya na ukame baada ya kukamilisha ziara ya siku mbili katika maeneo yaliiyoathika zaidi Somaliland.

Sauti
13'23"

21 Februari 2022

Leo ni siku ya kimataifa ya lugha mama. Lugha mama ni ile ambayo mtu anaizungumza ya kwanza na inaweza kuwa pale alikozaliwa au ni lugha ya asili ya jamii yake. Kwa wengi wa wakazi wa nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili ni lugha mama kwa kuwa inazungumzwa katika nchi zote za eneo hilo na zile za jirani na pia ni lugha ya kufundushia shuleni. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO linasema maudhui ya mwaka huu ya siku hii ni matumizi ya teknolojia katika kujifunza lugha mbalimbali, fursa na changamoto.

Sauti
12'15"

18 FEBRUARI 2022

Katija Jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa KLeah Mushi anakuletea

-Malawi imetangaza kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa polio nchini humo na hivyo kuwa ni tangazo la kwanza la uwepo wa ugonjwa huo barani Afrika katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano. 

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linashirikiana na mamlaka nchini Ethiopia na wadau wake kupatia msaada wa dharura kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Eritrea ambao walikimbia kambi ya Barahle na viunga vyake huko jimboni Afar baada ya mapigano kuibuka eneo hilo. 

Sauti
10'36"

17 Februari 2022

Hii leo tunaanzia Ukanda wa Sahel ambako wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yameshuhudia wakimbizi wakishiriki kwenye miradi ya kilimo na ujenzi wa nyumba ili kujipatia kipato. Kisha tunabisha hodi huko nchini Tanzania kumulika mradi wa uvuvi usioharibu mazingira unaotekelezwa na na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kupitia mradi wa FISH4ACP. Habari nyingine ni kuhusu tamasha la amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huko mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini.

Sauti
13'23"

15 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya saratani ya utotoni, 15 Februari 2022, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO barani ulaya limetoa ripoti inayoonesha kukosekana kwa usawa baina ya nchi na nchi kwa suala la saratani ya watoto katika Kanda ya Ulaya ya WHO. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO laonya kuhusu ukame unavyoongeza zahma ya kutokuwa na uhakika wa chakula Pembe ya Afrika. 

Sauti
12'10"

14 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

Ulimwengu ukiwa umeadhimisha siku ya redio duniani hapo jana na maudhui makuu yakiwa ni Imani kwa Radio, leo tunaiangazia redio iliyoanzishwa mnamo mwaka 1995 nchini Tanzania na huduma ya majesuit wa kikatoliki kwa wakimbizi (JRS), ili kuwakutanisha wakimbizi waliokuwa wamepoteana na jamaa zao wakati wa vita ya kimbari nchini Rwanda. 

Sauti
19'46"

11 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

Kujaa maji kwa ziwa Albert nchini Uganda kwaleta zahma kubwa kwa wakazi, wengine wapoteza makazi, Umoja wa Mataifa nao wanyoosha mkono kusaidia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vya chini vya wanawake wanaofanya kazi katika masuala ya Akili Bandia (AI), na kanuni za hovyo za upendeleo wa kijinsia. 

Sauti
12'38"

10 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo  

Niger yapongezwa kwakuonesha ukarimu kwa wasaka hifadhi na wakimbizi. Viongozi wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi na lile la Uhamiaji IOM Antonio Vittorino wamefanya ziara nchini humo. 

Timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuondokana na mabomu ya kutegwa ardhini, UNMAS pamoja na Mamlaka za Kitaifa wanafanya kazi kila siku nchini Sudan Kusini ili kuyadhibiti mabomu ambayo yako katika mazingira na hayajalipuka. 

Audio Duration
14'1"