Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 Februari 2022

23 Februari 2022

Pakua

Karibu kusikiliza jarida ambapo leo tutakuletea mada kwa kina kutoka viziwani Zanzibar nchini Tanzania , ambapo ikiwa imesalia chini ya miaka 8 kufikia ukomo wa malengo ya amendeleo endelevu SDG’s juhudi zinafanyika kwa hali na mali kuhakikisha jamii zinafikia malengo hayo. Miongoni mwa wanaharakati wa kupigia upatu malengo hayo ni mke wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Bi. Mariam Mwinyi ambaye mwishoni mwa wiki amezindua wakfu au taasisi maalum ijulikanayo kama “Zanzibar Maisha Bora Foundation”.

Pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa ufupi pamoja na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu Ukraine. 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
15'32"