Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

09 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo


Kuelekea siku ya kimataifa ya mikunde, vijana huko Kigoma kupitia mafunzo yaliyowezeshwa na Umoja wa Mataifa, wadhihirisha mikunde ni tija kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Sauti
13'36"

08 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

UNHCR, IOM, UNICEF na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, OHCHR, wasikitishwa sana na taarifa za kifo cha mtoto mchanga kilichotokea Jumapili wakati wa walinzi wa mpaka wa pwani wa Trinidad walipokuwa wanakizuia chombo kilichowabeba wavenezuela waliojaribu kuvuka mpaka. 

Sauti
14'26"

07 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

ikiwa ni siku moja baada ya ulimwengu kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana, FGM, tunaangazia harakati za Umoja wa Mataifa, wadau na wanaharakati katika kufanikisha kuelimisha umma kuhusu ubaya wa matendo hayo. 

Sauti
9'57"

Jarida 07 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 

ikiwa ni siku moja baada ya ulimwengu kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana, FGM, tunaangazia harakati za Umoja wa Mataifa, wadau na wanaharakati katika kufanikisha kuelimisha umma kuhusu ubaya wa matendo hayo. 

Sauti
9'57"

Jarida 04 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo 


Leah Mushi amefanya mazungumzo na Dokta. Paul Mutungi Afisa wa mashinani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO akihusika na wafugaji katika Ukanda wa Afrika wakiangazia suala la ukame na njaa kali unavyoathiri wananchi walioko Afrika Mashariki na pembe ya Afrika.


Mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi kwa mwaka huu wa 2022 yameng’oa nanga hii leo huko Beijing China huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akitoa wito wa mshikamano wakati wa michezo na hata baada.

Sauti
11'52"

Jarida 03 Februari 2022

Miongoni mwa yaliyomo


UNICEF yasaidia familia zinazokabiliwa na ukame na utapiamlo katika maeneo ya nyanda za chini nchini Ethiopia uliosababishwa na mvua kutonyesha katika misimu mitatu.


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaendelea kufanya kila jitihada kuwasaidia wakimbizi na raia wa Lebanon ambao wanakabiliana na moja ya misimu yenye baridi kali. 

Sauti
12'7"

Jarida 02 Februari 2022

Miongoni mwa tuliyonano kutoka UN


Leo ni mara ya kwanza kuadhimishwa kwa siku ya kimataifa ya maeneo oevu  tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio mwezi Agosti mwaka jana 2021. Tunabisha hodi nchini Laos kuona harakati za kuhifadhi maeneo hayo adhimu.


Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limelaani vikali mauaji ya watoto 15 katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Sauti
11'14"

Jarida 01 Februari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa 

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya inayoonesha kuwa mifumo ya usimamizi wa taka za afya duniani kote hivi sasa imezidiwa uwezo kutokana na maelfu ya tani za taka zinazotokana na vifaa vilivyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la COVID-19 na hivyo kutishia afya ya binadamu na mazingira na wakati huo huo kufichua hitaji kubwa la kuboresha udhibiti wa taka zinazozalishwa kutokana na huduma ya tiba. 

Sauti
13'3"

Jarida 31 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo kutoka Umoja wa Mataifa 

Wakimbizi wa Burundi walioishi kwa vipindi tofauti na hata miongo kadhaa ukimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR wameanza kurejea nyumbani Burundi. Kundi la kwanza katika mwaka huu wa 2022 waeleza furaha yao kurejea nchini mwao.  

Sauti
10'40"

Jarida 28 Januari 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo 

Jamii ya Maasai tarafa ya Liliondo, Wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha kaskazini mwa Tanzania waanza kuamia katika shughuli ngeni kwao, kilimo baada ya shughuli yao ya kitamaduni yaani ufugaji, kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi. 

Sauti
10'34"