Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 Februari 2022

16 Februari 2022

Pakua

Hii leo jaridani ni mada kwa kina ikimulika harakati za Umoja wa Mataifa kuhifadhi kidijitali nyaraka za zaidi ya miaka 100 za shirikisho la mataifa au League of Nations. Lakini kuna habari kwa ufupi zikiangazia mkutano wa kimataifa wa viongozi kuhusu watu wenye ulemavu, UNFPA Tanzania kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi nchini humo kukabili ukatili wa kingono na kijinsia ikiwemo ukeketaji na mwisho ni taarifa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM nchini Tanzania za kuhamishiwa nchi ya tatu kwa wakimbizi 57 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutoka Tanzania kwenda Marekani. Mashinani tunafunga safari hadi Mauritania kuona jinsi programu ya mlo shuleni imeleta mafanikio. Karibu na mwenyeji wako ni Leah Mushi.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'29"