Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 Februari 2022

14 Februari 2022

Pakua

Miongoni mwa yaliyomo 

Ulimwengu ukiwa umeadhimisha siku ya redio duniani hapo jana na maudhui makuu yakiwa ni Imani kwa Radio, leo tunaiangazia redio iliyoanzishwa mnamo mwaka 1995 nchini Tanzania na huduma ya majesuit wa kikatoliki kwa wakimbizi (JRS), ili kuwakutanisha wakimbizi waliokuwa wamepoteana na jamaa zao wakati wa vita ya kimbari nchini Rwanda. 

Hadi kufikia sasa watu 121 wameshapoteza maisha na wengine 29,000 wametawanywa kutokana na kuzuka kwa kimbunga Batsirai kilichoipiga Madagascar hivi karibuni. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa mpya zilizopokelewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umesema baada ya wiki kadhaa za kutoweka na kutokuwa na uhakika kuhusu waliko wanaharakati wanawake wanne na jamaa zao kumi na tisa, wanaharakati hao wameachiliwa na mamlaka. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na serikali ya Japan wametangaza ushirikiano mpya wa kuchangia dola milioni 1.25 kuisaidia serikali ya Ufalme wa Tonga kuhakikisha kuwa takriban watu 19,250 wakiwemo watoto 10,000 walioathiriwa na mlipuko wa volcano na tsunami hivi karibuni wanapata maji safi ya kutosha ya kunywa, mazingira safi, pamoja na afya njema. 

Na mashinani tutawasikia baadhi ya wasikilizaji wa redio wakieleza maoni yao kwa nini wanaona redio bado ni chombo wanachokitegemea sana. karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
19'46"