Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 Februari 2022

11 Februari 2022

Pakua

Miongoni mwa yaliyomo 

Kujaa maji kwa ziwa Albert nchini Uganda kwaleta zahma kubwa kwa wakazi, wengine wapoteza makazi, Umoja wa Mataifa nao wanyoosha mkono kusaidia. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vya chini vya wanawake wanaofanya kazi katika masuala ya Akili Bandia (AI), na kanuni za hovyo za upendeleo wa kijinsia. 

Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Mpango wa chakula Ulimwenguni , WFP kwa kushirikiana na serikali ya Madagascar yanaendelea kukimbizana na muda kuwasaidia watu katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga Batsirai nchini Madagascar hususani katika maeneo ya Mananjary na Manakara.   

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA imesema inayo furaha kutangaza kwamba Joyce Msuya raia wa Tanzania ameanza kazi rasmi kama Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Kibinadamu na Naibu Mratibu wa Misaada ya Dharura. 

Na leo katika neno la Wiki tunakwenda Nairobi, Kenya kupata ufafanuzi wa maana ya methali "NYIMBO ZA KUFUNZWA HAZIKESHI NGOMA” Karibu! 

Audio Duration
12'38"