Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 Februari 2022

17 Februari 2022

Pakua

Hii leo tunaanzia Ukanda wa Sahel ambako wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa yameshuhudia wakimbizi wakishiriki kwenye miradi ya kilimo na ujenzi wa nyumba ili kujipatia kipato. Kisha tunabisha hodi huko nchini Tanzania kumulika mradi wa uvuvi usioharibu mazingira unaotekelezwa na na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kupitia mradi wa FISH4ACP. Habari nyingine ni kuhusu tamasha la amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC huko mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini. Makala inabisha hodi mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako shirika la SAWA WANAWAKE Tanzania na hatua zake za kukabidhi majengo ya kusaidia kuepusha vitendo vya ukatili wa kijinsia.  Tunatamatisha na mashinani ambako tunafunga safari hadi nchini Haiti kusikia harakati za kunasua nchi hiyo baada ya tetemeko la ardhi. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'23"