Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 FEBRUARI 2022

18 FEBRUARI 2022

Pakua

Katija Jarida la mada kwa kina hii leo kutoka Umoja wa Mataifa KLeah Mushi anakuletea

-Malawi imetangaza kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa polio nchini humo na hivyo kuwa ni tangazo la kwanza la uwepo wa ugonjwa huo barani Afrika katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano. 

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linashirikiana na mamlaka nchini Ethiopia na wadau wake kupatia msaada wa dharura kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Eritrea ambao walikimbia kambi ya Barahle na viunga vyake huko jimboni Afar baada ya mapigano kuibuka eneo hilo. 

-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amehutubia mkutano wa kimataifa kuhusu masuala ya usalama huko Munich Ujerumani na kusema miaka mitatu tangu kufanyika kwa mkutano huo  bado dunia kwa bahati mbayá imezidi kuwa na changamoto na hatari zaidi .

-Mada yetu kwa kina leo inaangazia wito wa wanawake wa mji wa Mutwanga wilayani Beni nchini DRC baada ya kutembelewa na askari wanawake kutoka kikosi cha 8 cha walinda amani kutoka Tanzania  TANZBART 8 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO

-Na katika kujifunza Kiswahili tunabisha hodi Baraza la Kiswahili la Zanzibar BAKIZA kupata ufafanuzi wa methali  “Ndugu Chungu Jirani Mkungu."

 

Audio Credit
UN News? Leah Mushi
Audio Duration
10'36"