Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

19 OKTOBA 2022

Karibu kuungana na Assumpta Massoi anayekuletea jarida likiangazia masuala mbalimbali ikiwemo

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni limebainisha kuwa wagonjwa wa magonjwa yasiyo yakuambukiza kama vile utipwatipwa, kisukari na magonjwa ya moyo wanazidi kuongezeka duniani na serikali zitaingia gharama kubwa iwapo hazitaongeza nguvu katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ya mwili.

Sauti
12'14"

18 OKTOBA 2022

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anakuletea Mada Kwa Kina kuhusu harakati za Umoja wa Mataifa za kutokomeza umaskini kwenye mkoa wa Kigoma nchini Tanzania kupitia mashrika yake yanayotekeleza Mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP lakini pia kuna Habari kwa Ufupi zikimulika:

Sauti
11'43"

17 Oktoba 2022

Karibu kusikiliza jarida, Flora Nducha anakuletea yale yaliyojiri kutoka Umoja wa Mataifa ikiwemo;- 

1. Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga umasikini ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema lazima hatua za dharura zichukuliwe, tena kwa kuzingatia watu na utu. 

2. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF nchini Uganda kwakushirikiana na serikali ya Japan wanaisaidia serikali ya Uganda kuimarisha mifumo ya afya ili watoto wote waweze kupata chanjo. 

Sauti
11'32"

13 OKTOBA 2022

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Dunia ipo hatarini kuingia katika mwaka mwingine wenye uhaba wa chakula wakati huu ambapo watu wengi tayari wanazidi kuingia katika dimbwi la uhaba wa chakula, limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP ambalo limetoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa kushughulikia mzizi wa tatizo hili wakati dunia ikielekea kuadhimisha siku ya chakula duniani hapo Oktoba 16.

Sauti
12'35"

12 OKTOBA 2022

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo utasikia taarifa kuhusu Mradi wa kusaidia wanawake katika sekta ya kilimo nchini Tanzania unaotekelezwa na mashirika manne ya Umoja wa Mataifa. 

Pia utasikia IMF yaeleza kuhusu uchumi wa dunia kuzorota. 

Katika upande wa makala utasikia kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya watoto. 

Karibu uungane na Flora Nducha kusikiliza. 

Sauti
14'7"

11 OKTOBA 2022

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Umoja wa Mataifa umeshtushwa na ongezeko kubwa la wakimbizi wa ndani huko magharibi kwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC baada ya kuibuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwezi Julai huko Kwamouth.

Sauti
10'44"

10 OKTOBA 2022

Hii leo kwenye Habari za UN Flora Nducha anamulika afya ya akili, masuala ya uchumi ili kujenga amani pamoja na huduma za kujisafi na usafi.

1. Siku ya afya ya akili duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema kunawahudumu wawili tu wa afya ya akili katika kila watu 100,000 na athari za kijamii na kiuchumi za janga hili ni kubwa mno.

2. Mradi wa Umoja wa Mataifa nchini Sri Lanka wainua uchumi wa watu wa jamii ya watamili na kusaidia kujenga amani.

Sauti
10'50"

07 OKTOBA 2022

Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa  limesema Pamba ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa mataifa mbalimbali duniani, hivyo hatua Madhubuti zinahitajika kuhakikisha zao hilo linaendelezwa na wakulima wake kulindwa dhidi ya changamoto lukuki ikiwemo mabadiliko ya tabianchi

Sauti
12'26"

06 OKTOBA 2022

Hii leo katika Habari za UN Assumpta Massoi anakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Kujifunza Lugha ya Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi kuna haki za mtoto kuzingatiwa hasa wakati huu ambapo majanga ya kiasili na yanayosababishwa na binadamu  yanakengeua utekelezaji wa haki za mtoto. Suala la afya ya akili barani Afrika ambayo inachochea matukio ya kujiua ,na WHO imezindua kampeni maalum. Na kisha ni uzinduzi wa ripoti kuhusu matumizi ya matukio makubwa ya michezo ili kuimarisha afya ya mwili ya binadamu.

Sauti
11'26"