Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 OKTOBA 2022

18 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anakuletea Mada Kwa Kina kuhusu harakati za Umoja wa Mataifa za kutokomeza umaskini kwenye mkoa wa Kigoma nchini Tanzania kupitia mashrika yake yanayotekeleza Mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP lakini pia kuna Habari kwa Ufupi zikimulika:

  • Huko Berlin, Ujerumani kando mwa mkutano wa viongozi kuhusu afya, viongozi wa dunia wamethibitisha kuwa watatoa dola bilioni 2.6 kusaidia mpango wa kimataifa wa kutokomeza polio duniani, GPEI, wa kuanzia mwaka huu wa 2022 hadi 2026.  
  • Vita, mizozo, COVID-19 vlivyodumaza mafanikio ya ustawi wa afya ya wanawake, watoto na vijana.
  • Na leo ni siku ya kimataifa  kuhusu kukoma kwa hedhi kwa wanawake au Menopause kwa lugha ya kiingereza maudhui yakiwa uelewa na fikra ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema hali hiyo inaathiri kiuchumi na kijamii zaidi ya nusu ya wakazi wa dunia lakini uelewa wake bado ni mdogo, hivyo linataka serikali kutambua suala hilo kuwa la afya ya umma

Na kutoka mashinani, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni Irene Khan anasema mataifa mengi wakati wa vita hutumia kutoa Habari kama njia moja wapo ya kuleta mgawanyiko, chuki, kuchochea ghasia, kudhalilisha watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa Habari na hali imekuwa mbaya wakati huu ambapo teknolojia ya kidijitali inawawezesha kufikia watu wengi zaidi.

Karibu!

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
11'43"