Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 OKTOBA 2022

06 OKTOBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN Assumpta Massoi anakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Kujifunza Lugha ya Kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi kuna haki za mtoto kuzingatiwa hasa wakati huu ambapo majanga ya kiasili na yanayosababishwa na binadamu  yanakengeua utekelezaji wa haki za mtoto. Suala la afya ya akili barani Afrika ambayo inachochea matukio ya kujiua ,na WHO imezindua kampeni maalum. Na kisha ni uzinduzi wa ripoti kuhusu matumizi ya matukio makubwa ya michezo ili kuimarisha afya ya mwili ya binadamu.

Mada kwa kina ni kijana Jessica Mshama, Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akizungumzia alichojifunza wakati wa Mkutano wa ngazi ya juu wa  Umoja wa Mataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa elimu.

Na kwenye kujifunza Kiswahili ni uchambuzi kutoka Kenya wa methali isemayo, Kinga na Kinga ndipo moto huwaka! Karibu

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
11'26"