Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

17 JANUARI 2022

Tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa

Shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO limeonya mwaka 2022 ukuaji wa sekta ya ajira unatarajiwa kuzorota na tena bila uhakika kutokana na kuendelea kuwepo kwa janga la COVID-19 ambalo limeathiri soko la nguvukazi ulimwenguni.

Sauti
11'10"

14 JANUARI 2022

Machache kati ya mengi tuliyokuandalia hii leo kutoka UN

WHO yapendekeza dawa mbili mpya za kutibu wagonjwa wa COVID-19 ambazo ni Baricitinib ya kumeza kwa ajili ya kutibu wagonjwa mahututi  wa COVID-19 na nyingine ni Sotrovimab ya sindano ambayo ni kwa ajili ya wagonjwa wasio katika hali mbaya sana.

Na katika mada kwa kina tunaelekea mkoani  Ruvuma nchini Tanzania kumulika mradi wa nishati salama uliofanikishwa na Umoja wa Mataifa kwa kuwaunga mkono wenyeji.

Sauti
11'14"

13 JANUARI 2022

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo katika habari za Umoja wa Mataifa


Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO linasema kuwa japokuwa habari mbayá ni kuwa Omicron ambao ni mnyumbuliko wa virusi vya corona ulichochea wimbi la nne la Covid-19 barani Afrika lakini unapungua haraka kuliko mawimbi yaliyotangulia kama lile la mnyumbuliko aina ya Delta. Hata hivyo idadi ya waliopata chanjo dhidi ya Covid-19 barani humo baado ni ndogo mno.  

Sauti
12'31"

12 JANUARI 2022

Miongoni mwa tuliyonayo katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa: 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau kama shirika la SIDA na shirika lisilo la kiserikali AVSI wamewezesha uboreshaji wa sekta ya afya hasa kwa katika mkoa wa West Nile nchini Uganda.

Sauti
13'18"
UN/ John Kibego

Wito wetu kwa DRC ni amani tu ili siku moja turejee nyumbani – Wakimbizi Uganda 

 

Ugenini ni ugenini tu na japokuwa Uganda tunapapenda lakini DRC ikipata amani tutafurahi kurudi kwetu. Hivyo ndivyo wanavyosema wakimbizi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoishi katika kambi za wakimbizi zilizoko nchini Uganda wakiguswa na hali ya usalama katika majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini ikiwa ni zaidi ya muongo mmoja sasa wakiwa ukimbizini katika nchi ya jirani, Uganda. 

Wakimbizi hao raia wa DRC wanasema mara kwa mara wanafuatilia hali ya amani katika nchi yao kwa imani kuwa siku moja amani itatangazwa ili warejee makwao. 

Sauti
2'38"

11 JANUARI 2022

UN yazindua mpango wa kusaidia wananchi wa Afghanistan.


DNA za walinda amani wa Afrika Kusini huko DRC zakusanywa kubaini baba za watoto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.


Washirika wa Kimataifa wa Somalia wahimiza kukamilika haraka kwa mchakato wa Uchaguzi.
 

Sauti
12'51"

07 JANUARI 2021

Katika mada kwa kina tunamwangazia Mwanaharakati msichana Zulaikha Patel wa Afrika Kusini aliyeanza kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi akiwa na umri wa miaka 13 katika shule ya sekondari ya wasichana mjini Pretoria.

Sauti
9'57"

05 JANUARI 2022

Ni Jumatano ya tarehe 05 mwezi Januari mwaka 2022 leo tunakuletea mada kwa kina kutoka nchini Rwanda kumulika hatua za taifa hilo za kutekeleza mkataba wa kimataifa wa wakimbizi.

Pia utapata fursa ya kusikiliza habari kwa ufupi zikiangazia masuala mbalimbali ikiwemo UNESCO kulaani mauaji ya mwandishi wa habari nchini Myanmar. 

 

Sauti
9'59"