UNMISS na UNICEF walaani mauaji nchini Sudan kusini
Ujumbe wa kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umelaani vikali shambulio lililotokea jumapili tarehe 23 Januari 2022 huko Baidit, Jimbo la Jonglei na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30, majeruhi kadhaa, wananchi wengine kufururushwa katika makazi yao na nyumba kuchomwa moto.