Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabaki ya silaha za vita yaliyozagaa Sudan Kusini ni tishio kubwa la usalama wa raia:UNMAS 

UNMAS wakitegua mabomu katika eneo la Equatoria mashariki nchini Sudan Kusini. Pichani ni eneo shambani ambako kilipuzi kimebainika
UNMISS\Nektarios Markogiannis
UNMAS wakitegua mabomu katika eneo la Equatoria mashariki nchini Sudan Kusini. Pichani ni eneo shambani ambako kilipuzi kimebainika

Mabaki ya silaha za vita yaliyozagaa Sudan Kusini ni tishio kubwa la usalama wa raia:UNMAS 

Amani na Usalama

Nchini Sudan Kusini wakati sasa milio ya risasi inaweza kuwa imepungua katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo, jinamizi la vita vya wenyewe kwa wenyewe bado linawaandama hasa kwa kuzagaa kwa manbaki ya silaha za vita kama mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya mlipuko, ambavyo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayochukua hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS ni tishio la kila siku kwa maisha ya wanawake, watoto na wanaume kwenye maeneo mbali mbali nchini humo 

Katika eneo la Ngulere jimboni Equatoria ya Kati Sudan Kusini hali ni Dhahiri kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea kwa zaidi ya miaka 10 sasa vimeacha alama, na hasa mabaki ya silaha za kivita ikiwemo mabomu ya kutegwa ardhini. 

Wafanyakazi wa UNMAS wako hapa kwa kampeni maalum ya kukusanya mabadi ya silaha hizo kuanzia mashambani hadi kwenye viwanja vya michezo ili kuwahakikishia usalama watu wa taifa hili changa zaidi duniani. 

UNMAS imekuwa Sudan Kusini tangu mwaka 2004 likisafisha mabaki ya silaka katika eneo lenye kilometa za mraba milioni 45. 

Na hapa Ngulere wamekuwa wakisafisha mabaki ya silaha hizo kwenye uwanja wa kandandanda ambao sasa ni salama kwa watoto kucheza kupitia mradi maalum wa viwanja salama ambao unaziunganisha jamii kupitia michezo. Rebecca Bellrose ni afisa wa program wa UNMAS 

"Mpango wa viwanja salama ni mpango wa miaka mitano ambao ulianza mnamo 2019 na unamalizika mnamo 2023. Lengo kubwa la mpango huu au kwa kampeni hii ni kugeuza viwanja vya mabomu kuwa viwanja vya michezo. Baada ya kusema hayo, tunaona maeneo yaliyochafuliwa na mabomu yako karibu na shule, au viwanja vya michezo au mahali watoto wanapokutana, na tunaondoa uchafu huo. " 

 Kwa wakaazi,  eneo hili kuondolewa kwa mabomu hayo yenye historia ya umwagaji damu kutahakikisha biashara inashamiri, watoto wanastawi, na watu wanaweza kuishi bila woga.  

Na kwa timu ya UNMAS, ni wakati wa kujionea mwenyewe matunda ya kazi yao kwa maisha ya jamii ambazo wako hapo kuzilinda.