Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa ufugaji wa Samaki umenikombia mimi na familia yangu: Michael Chiwayi

Mradi wa ufugaji wa Samaki umenikombia mimi na familia yangu: Michael Chiwayi

Pakua

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi unafanyika leo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu , UNGA78 lengo likiwa kuzihamasisha nchi wanachana kuchukua hatua zaidi kuzinusuru nchi zinazobeba mzigo mkubwa wa athari za janga hilo. Eneo la Kibokoni kaunti ya Kilifi nchini Kenya ni moja ya maeneo ya wavuvi yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi na kuwalazimu wavufi kutafuta mbinu mbadala ya kuweza kujikimu kimaisha.  Na ndipo chini ya mwamvuli wa shirika lisilo la kiserikali la Umoja Self-Help Group likiwa na wanachama 40 wakaanzisha mabwa 17 ya ufugaji wa Samaki aina ya milkfish, dagaa kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na tilapia wa baharini. Mradi huu unaihakikisha jamii uzalishaji, kuwainua kiuchumi  na kuwajengea mnepo. Tuungane Flora Nducha na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo katika makala hii iliyofanikishwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS, Nairobi Kenya.

Audio Credit
Selina Jerobon/Flora Nducha
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
UNIS Nairobi