Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jiungeni na EAC tupate nguvu zaidi ya kuweza kuwasaidia

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki.
UN News
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki.

Jiungeni na EAC tupate nguvu zaidi ya kuweza kuwasaidia

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki amezisihi nchi nyingi zaidi zilizopo katika ukanda huo kujiunga na jumuiya yao ili waweze kuwa na nguvu zaidi na pale zitakapokumbwa na changamoto waweze kuwasaidia kwa karibu zaidi kama jumuiya. 

Akizungumza katika mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dkt. Mathuki ametolea mfano nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambayo ilijiunga na jumuiya hiyo mwaka jana 2022 na kusema kuwa wanaweza kuwasaidia lakini nchi kama Sudan ambayo bado haijawa mwanachama wanashindwa.

“Hizi nchi zote ukiziangalia mfano Sudan, Ethiopia na Djibout zote zikijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki kutakuwa na uwezekano tutakuwa na jumuiya yenye nguvu zaidi na ikiwa tutapata changamoto yoyote kwa pamoja tutaweza kuzitatua zile changamoto.” 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki amezungumza na Leah Mushi WA Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
UN News
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki amezungumza na Leah Mushi WA Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

Malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)

Wakati Mkutano wa Malengo ya maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa ukiingia katika siku yake ya pili hii leo katika makao Makuu, Dkt. Mathuki ameeleza kuwa EAC wanafanya juhudi mbalimbali kuhakikisha wanatimiza malengo hayo. 

Ametaja mikutano miwili iliyofanyika hivi karibuni, mmoja nchini kenya kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na mwingine nchini Tanzania kuhusu kilimo, wakuu wote wa nchi hizo wamesisitiza haja ya kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwani linaathiri pia sekta nyingine. 

“Ukiangalia mambo ya elimu, chakula yote yanaathiriwana mabadiliko ya tabianchi na hiyo yote inaathiriwa na nchi zilizo endelea.” Alieleza Dkt .Mathuki huku akitoa wito kwa nchi hizo kutoa fedha walizoahidi za mnepo wa mabadiliko ya tabianchi. 

Mtendaji huyu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pia amesema si sawa kulinganisha nchi zilizoendelea na zile zinazo endelea kwani nchi zinazoendelea bado zinashughulika na changamoto nyingi za kimsingi ukilinganisha na zile zilizoendelea ambazo hazina shida hizo.