Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Watoto wakiangalia nyumba yao iliyosambaratishwa kwenye mji wa Rafah Kusini mwa Gaza
© UNICEF/Eyad El Baba

Wiki 10 za jinamizi kwa watoto Gaza: UN

Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati ni mahali pa hatari zaidi duniani kuwa mtoto na vifo vya vijana kutokana na maradhi huenda vikapita vile vya mashambulizi ya mabomu bila kuwepo kwa usitishaji mapigano, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.

UNICEF inawasaidia watoto waliokimbia makazi yao huko Gaza kutabasamu na kurejesha matumaini kwa kuandaa shughuli za burudani katika makazi. (Maktaba)
Photo: UNICEF/Loulou d'Aki

Habari kwa ufupi: Gaza, Sudan, Mifumo ya chakula

Leo Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Gaza ni mahali hatari zaidi kuishi kwa watoto. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, James Elder amesema  “Siku baada ya siku ukatili wa hali ya juu unadhihirika. Katika saa 48 zilizopita hospitali kubwa Zaidi iliyobaki inafanyakazi imeshambuliwa mara mbili. Hospitali hiyo ya Al Nasser iliyopo Khan Yunis sio tu kwamba inahifadhi idadi kubwa ya Watoto ambao tayari wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi majumbani kwao lakini pia inahifadhi mamia ya wanawake na Watoto wanaosaka usalama.”

Afisa Habari wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO ofisi ya Beni jimboni Kivu Kaskazini akipatia mafunzo wanahabari, wanaharakati na wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuhusu habari potofu na habari za uongo mjini Beni.
UN./George Musubao

MONUSCO imetuepusha kutumbukia kwenye usambazaji wa habari za uongo na potofu- Wanufaika

Kesho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni uchaguzi mkuu ikiwa ni tamati ya kampeni huku Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umeshiriki kwa kusafirisha sio tu vifaa vya uchaguzi lakini pia kuelimisha wananchi jinsi ya kukabili na kuzia habari potofu na za uongo kwani ni tisho la amani na usalama.