Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

WHO lazindua Baraza jipya la vijana
WHO / Chris Black

WHO lazindua Baraza jipya la vijana

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezindua Baraza la vijana lililofanyika kuanzia tarehe 27- 30 Januari 2023 jijini Geneva Uswisi na kuwaleta pamoja viongozi vijana kutoka mashirika 22 ya vijana duniani yanayojishughulisha na masuala ya afya na masuala yasiyo ya afya.

Waudumu wa WHO wakiwa kwenye shughuli katika kambi ya kanyaruchinya wilayani Nyiragongo-Goma
UN News/ Byobe Malenga.

Chanjo dhidi ya Kipindupindu yaendelea Kivu Kaskazini, DRC- WHO

Kampeni ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu  iliyoanza tarehe 25 mwezi huu huko Kivu Kaskazini nchini jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC imekunja jamvi jana Jumanne ya tarehe 30 mwezi hu uwa Januari ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO lilizindua kampeni hiyo ya chanjo kwa wakimbizi wa ndani katika kambi ya wakimbizi hao ya Kanyaruchinya wilayani nyiragongo katika mji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini.

Sauti
5'30"
Jamii ya Benet nchini Uganda ambao bado hawana Utaifa.
UNHCR Video

Jamii ya Benet nchini Uganda yaiomba serikali kumaliza changamoto yao ya kutokuwa na utaifa: UNHCR

Baada ya zaidi ya takriban miongo minane ya kutokuwa na utaifa, jamii ya watu wa asili ya Benet nchini Uganda inahaha kuishi, na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bila kuwa na nyaraka rasmi muhimu haiwezi kupata huduma za msingi kama elimu na afya , na sasa jamii hiyo inaiomba serikali ya Uganda kumaliza zahma hiyo iliyowaghubika kwa miongo.

Sauti
3'6"