Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Kutoka Maktaba: Hugh Masekela akitumbuiza katika uzinduzi wa siku ya kimataifa ya Jazz kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa New York, 30 Aprili 2012
UN Photo/JC McIlwaine

Muziki wa jazi umesongesha amani na kusikilizana- UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya muziki wa jazi duniani, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay ametoa ujumbe wake kwa kukumbusha jinsi karne moja iliyopita, mwanamuziki Joe Oliver al-maaruf King na bendi yake ya Creole, alivyotoa wimbo wake ambamo kwao tarumbeta na buruji alizotumia zilikuwa ndio kichocheo cha mustakabali wa muziki wa jazi hadi hii leo.

Mwambata wa jeshi Brigedia Generali Absolomon Lyanga Shausi akisalimiana na Afisa wa Polisi wa NEPAL iliyopo chini ya MINUSCA mara baada ya kumaliza ziara yake ya kujitambulisha kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanahudumu chini ya MINUSCA nchini CAR.
TANBAT 6

Mwambata jeshi wa Tanzania nchini CAR asifu utimamu wa wanajeshi wa Tanzania

Mwambata jeshi wa Tanzania anayehudumu kazi yake Jamhuri ya Afrika ya kati Brigedia Jenerali Absolomon Lyanga Shausi amefanya ziara ya kutembelea kikosi cha walinda amani wa Tanzania TANBAT6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA ili kujitambilisha tangu kikosi hicho kianze shughuli ya ulinzi wa amani kikipokea majukumu kutoka kwa kikosi cha TANBAT5 mwishoni mwa mwaka jana.

Sauti
2'31"
Usugu wa dawa kwa viua vijiumbe maradhi hutokea pale vijiumbe maradhi kama vile bakteria au vimelea, virusi na wengineo wanapokuwa wamebadilika katika kipindi fulani na hivyo hawawezi tena kutibika kwa kutumia dawa zilizoko
© WHO/Etinosa Yvonne

Maabara walimo wapiganaji Sudan kuna vimelea hatari ikiwemo TB sugu

Taarifa za sitisho la mapigano Sudan zikipokelewa kwa shangwe, shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Mediteranea Mashariki limeyataka makundi yanayozozana kuondoka kwenye maabara kuu ya afya ya umma nchini humo kwa kuwa kitendo hicho kinahatarisha kusambaa kwa vijidudu hatari vya magonjwa vilivyohifadhiwa kwenye maabara hiyo.